Uzalishaji wa msamiati katika mradi wa microsoft East Africa 2004-2009
dc.contributor.author | Mabeya, Moraa Jackline | |
dc.date.accessioned | 2012-07-06T08:03:47Z | |
dc.date.available | 2012-07-06T08:03:47Z | |
dc.date.issued | 2012-07-06 | |
dc.description | Department of Kiswahili and African Languages: 173p. The QA 76.754 .M3 2012 | |
dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia suala la matumizi ya Kiswahili katika mradi wa Microsoft East Africa. Umebainisha mbinu zilizohusika katika uundaji wa msamiati katika mradi huu. Aidha, umechunguza jinsi mbinu ambazo zilitumika zimechangia katika kukikuza na kukiendeleza Kiswahili kama lugha ya teknolojia. IIi kufanikisha kazi hii, mtafiti ametumia nadharia ya tafsiri kama nadharia msingi iliyochangiwa na Cartford (1965), vigezo vya PEGITOSCA na Kiingi (1989) na mhimili mmoja kutoka nadharia ya Msambao wa Uvumbuzi iliyoasisiwa na Everret (1962). Nadharia ya Tafsiri kwa mtazamo wa kiisimu hushughulikia kubadilisha vipashio vya kiisimu na sarufi. Vipashio hivi ni vya matini chasili hadi vile vya matini lengwa. K wa hivyo tafsiri hutendeka katika viwango vya kiisimu na sarufi. Nadharia hii hujishughulisha najinsi dhana zinavyopata msamiati. Nadharia ya Msambao wa uvumbuzi hujaribu kueleza jinsi teknolojia mpya mbalimbali zinavyosambaa katika jamii kupitia lugha za jamii husika. Vigezo vya PEGITOSCA m vigezo ambavyo hutumiwa kutathmini ufaafu wa msamiati uliozalishwa katika lugha husika. Data ya utafiti huu ilipatikana kwenye mtandao na nyanjani. Mtafiti alitumia sampuli elekezi na mahojiano ili kufikia malengo ya utafiti huu. Utafiti huu ulitarajiwa kuziweka wazi mbinu za uzalishaji wa msamiati katika kukishirikisha Kiswahili kwenye mradi wa Microsoft East Africa. Utafiti huu ulitumia msamiati takribani 194. Data imechanganuliwa kwa kutumia mihimili ya nadharia zilizotajwa hapo juu. Utafiti uliweza kutibitisha kwamba baadhi ya msamiati uliozalishwa umepungukiwa kinadharia. Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kiteknolojia sasa na inahitaji kushughulikiwa kwa makini sana. Kazi hii ina jumla ya sura tano.Sura ya kwanza ni utangulizi wa tasnifu hii, sura ya pili inajadili ushirikishi wa Kiswahili katika mradi wa Microsoft East Africa, sura ya tatu inajadili mbinu zilizotumika katika kuzalisha msamiati, sura ya nne ni uchanganuzi wa data nayo sura ya tano inahusu matokeo ya utafiti. | en_US |
dc.description.sponsorship | Kenyatta University | en_US |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/5291 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.subject | Computer software | |
dc.subject | Africa, East | |
dc.subject | Microsoft software | |
dc.subject | Computer software industry | |
dc.subject | Swahili language | |
dc.title | Uzalishaji wa msamiati katika mradi wa microsoft East Africa 2004-2009 | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Uzalishaji wa msamiati katika mradi wa microsoft East Africa 2004-2009.pdf
- Size:
- 90.12 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full Text Thesis
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 2.68 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: