Show simple item record

dc.contributor.authorWanjala, Fred Simiyu
dc.date.accessioned2014-04-22T08:31:14Z
dc.date.available2014-04-22T08:31:14Z
dc.date.issued2014-04-22
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/9403
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages, 105p. The PL 8092.B87 W3 2007en_US
dc.description.abstractUtafiti huu unachunguza maudhui na lugha katika nyiso za Wabukusu. Unachunguza namna fanani hubadilisha lugha na maudhui katika nyizo za Wabukusu ili kutekeleza madhumuni yake. Utafiti unajikita katika nyimbo zilizoimbwa katika vipindi viwili tofauti vya kihistoria: Bamaina (1960-1970) na Bakolongolo (2000-2010). Utafiti umechanganua nyimbo katika vipindi hivi kwa kuzingatia mabadiliko na maendeleo yaliyojiri wakati huo. Maendeleo na mabadiliko yalijikita katika asasi muhimu kama ndoa, elimu, siasa, uchumi na maingiliano ya kijamii. Utafiti wetu umebainisha kuwa watunzi huzingatia vipengele mbalimbali wakati wa kutunga na kuimba nyimbo za tohara. Vipengele hivi ni kama muktadha, jukwaa la tukio, hadhira lengwa, washiriki, namna ya uwasilishaji, sifa za fanani na sajili husika. Mazingatio haya huzipa nyimbo wajibu wake. Kwa kuzingatia vipengele hivi, watunzi hubadili lugha na maudhui ili kuzipa nyimbo umuhimu na utendaji kazi wake. Kazi hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi unaojadili swala la utafiti, misingi ya nadharia, sababu za kuchagau mada, yaliyoandikwa juu ya mada, upeo wa utafiti na mbinu za utafiti. Sura ya pili imejadili historia ya tohara katika jamii ya Wabukusu. Sura hii imeangazia chimbuko la tohara miongoni mwa Wabukusu kuanzia mwaka wa 1748. Utafiti umelenga maendeleo na mabadiliko katika nyimbo tangu mwaka wa 1748 hadi sasa. Vipengele ambavyo vilizingatiwa ni maudhui, lugha na utendaji kazi wa nyimbo katika vipindi tofauti vya kihistoria. Aidha, uratibu wa hirimu (bibingilo) kwa mujibu wa maendeleo na mabadiliko katika jamii tangu kuasisi kwa tohara umezingatiwa. Sura ya tatu imechanganua nyimbo zilizoimbwa wakati wa 'Bamaina' (kati ya miaka 1960 - 1970). Nyimbo tano zimechanganuliwa kwa kuzingatia vipengele vya maudhui, lugha na utendaji) kazi wake. Imebainika kuwa nyimbo zilitungwa na kuimba ili kusawiri na kumulika yaliyojiri katika jamii katika kipindi hiki. Sura ya nne imechanganua nyimbo zinazoimbwa katika kipindi cha 'Bakolongolo' wa sasa (2000-2010). Nyimbo tano zimechanganuliwa kwa mujibu wa maudhui, lugha na utendaji kazi wake. Tumeng'amua kwamba, watunzi nyimbo huteua maudhui na lugha kwa kuzingatia maendeleo na mabadiliko yanayotokea katikajamii. Sura ya mwisho ni hitimisho. Katika sehemu hii tumebainisha mazingatio wanayoyatilia maanani watunzi wa nyimbo za tohara katika jamii ya Wabukusu. Mazingatio haya yamezifanya nyimbo kutimiza malengo yake kwa kubadili lugha na maudhui kwa mujibu wa muktadha na wakati. Katika sura hii, pia maelezo yametolewa kwa mukhtasari. Muhtasari, matokeo, mapendekezo na matatizo yaliyojiri wakati wa utafiti wetu. Aidha, kuna mapendekezo na matatizo yaliyotufika wakati wa utafiti.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isootheren_US
dc.subjectCircumcision--songs and musicen_US
dc.subjectInitiation rites--KUSU--Kenyaen_US
dc.titleNyiso za wabukusu: maudhui na lughaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record