Show simple item record

dc.contributor.authorMusyoka, Esther Eunice
dc.date.accessioned2012-07-24T08:24:38Z
dc.date.available2012-07-24T08:24:38Z
dc.date.issued2012-07-24
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/5373
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages Department: 140p. The ML 3760.5 .M8 2012
dc.description.abstractUtafiti huu ulidhamiria kufafanua tamathali za lugha zinazotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa katika muktadha wa mazishi ya Kikristo ya jamii ya Wakamba, wakati wa kuwasilisha ujumbe kupitia nyimbo. Lugha iliyotumiwa katika nyimbo hizo huwa teule na yenye ukwasi mkubwa wa tamathali za usemi kama vile: jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi, takriri na maswali ya balagha miongoni mwa zingine. Kimsingi matumizi hayo huvuta hisi za hadhira kwa njia ya pekee. Aidha, utafiti huu ulilenga kubainisha ujumbe unavyowasilishwa kupitia tamathali za lugha, ili kuibua mielekeo yajamii ya Wakamba kuhusu kifo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mtindo na ya Ethnografia ya Mawasiliano. Mihimili mitatu ya nadharia ya Mtindo namhimili mwingine mmoja wa Ethnografia ya Mawasiliano iliunganishwa ili kuunda mihimili minne mahususi iiiyotumiwa katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa ili kubainisha dhima ya matumizi ya tamathali za lugha katika uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo za mazishi ya Kikristo ya Wakamba. Aidha utamaduni wa jamii hii haujadidimia kabisa kwa sababu, athari yake bado ina nguvu katika jamii. Maoni hayo yamedhihirishwa kupitia kwa mielekeo inayoibuliwa na kauli teule katika nyimbo hizo. Kwa ambavyo utanzu wa nyimbo za mazishi haujafanyiwa utafiti wa kina katika jamii ya Wakamba, utafiti huu umetoa mchango kuhusu utanzu huo wa fasihi simulizi. Kwa vile umefanunua baadhi ya tamathali muhimu za lugha zilizoshirikishwa katika uwasilishaji wa utanzu huu katika eneo la Thaana Nzau. Data ilikusanywa nyanjani katika wilaya ya Migwani, tarafa ya Thaana Nzau. Udurusu wa vitabu na majarida maktabani ulisaidia katika kupata maelezo ya baadhi ya tamathali za lugha, na jinsi ya kuzitumia katika muktadha wake. Mbinu ya ukusanyaji wa data ilizingatia uchanganuzi- shirikishi pamoja na mahojiano, Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia tamathali maalum za lugha, ujumbe, malengo ya utafiti na mihimiii ya nadharia zilizozingatiwa Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isoenen_US
dc.subjectFolk music
dc.subjectKenya
dc.subjectKamba (African tribe)
dc.subjectSocial life and customs
dc.titleUhakiki wa kimtindo wa nyimbo za mazishi miongoni mwa wakambaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record