• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Uhakiki wa kimtindo wa nyimbo za mazishi miongoni mwa wakamba

Thumbnail
View/Open
Full text Thesis (81.62Mb)
Date
2012-07-24
Author
Musyoka, Esther Eunice
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu ulidhamiria kufafanua tamathali za lugha zinazotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa katika muktadha wa mazishi ya Kikristo ya jamii ya Wakamba, wakati wa kuwasilisha ujumbe kupitia nyimbo. Lugha iliyotumiwa katika nyimbo hizo huwa teule na yenye ukwasi mkubwa wa tamathali za usemi kama vile: jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi, takriri na maswali ya balagha miongoni mwa zingine. Kimsingi matumizi hayo huvuta hisi za hadhira kwa njia ya pekee. Aidha, utafiti huu ulilenga kubainisha ujumbe unavyowasilishwa kupitia tamathali za lugha, ili kuibua mielekeo yajamii ya Wakamba kuhusu kifo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mtindo na ya Ethnografia ya Mawasiliano. Mihimili mitatu ya nadharia ya Mtindo namhimili mwingine mmoja wa Ethnografia ya Mawasiliano iliunganishwa ili kuunda mihimili minne mahususi iiiyotumiwa katika uchanganuzi wa data. Utafiti huu ulifanywa ili kubainisha dhima ya matumizi ya tamathali za lugha katika uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo za mazishi ya Kikristo ya Wakamba. Aidha utamaduni wa jamii hii haujadidimia kabisa kwa sababu, athari yake bado ina nguvu katika jamii. Maoni hayo yamedhihirishwa kupitia kwa mielekeo inayoibuliwa na kauli teule katika nyimbo hizo. Kwa ambavyo utanzu wa nyimbo za mazishi haujafanyiwa utafiti wa kina katika jamii ya Wakamba, utafiti huu umetoa mchango kuhusu utanzu huo wa fasihi simulizi. Kwa vile umefanunua baadhi ya tamathali muhimu za lugha zilizoshirikishwa katika uwasilishaji wa utanzu huu katika eneo la Thaana Nzau. Data ilikusanywa nyanjani katika wilaya ya Migwani, tarafa ya Thaana Nzau. Udurusu wa vitabu na majarida maktabani ulisaidia katika kupata maelezo ya baadhi ya tamathali za lugha, na jinsi ya kuzitumia katika muktadha wake. Mbinu ya ukusanyaji wa data ilizingatia uchanganuzi- shirikishi pamoja na mahojiano, Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia tamathali maalum za lugha, ujumbe, malengo ya utafiti na mihimiii ya nadharia zilizozingatiwa Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/5373
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback