Ulemavu wa usemi na lugha: Changamoto kutokana na kigugumizi katika ujifunzaji shuleni
Abstract
Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza changamoto za kigugumizi katika ujifunzaji shuleni. Uliwalenga watoto wa kati ya miaka mitatu hadi kumi kwa kuwa hiki ndicho kipindi muhimu cha ukuaji wa lugha, Watafitiwa walikuwa wanafunzi na walimu katika Manispaa ya Kisii. Mbinu za hojaji, kushuhudia na mahojiano zilizotumiwa kukusanya deta muhimu. Ilibainika kuwa wanaogugumiza hukumbwa na changamoto kadha kwa kuwa usemi ni muhimu katika ujifunzaji wa kiwango hiki cha watoto. Utafiti ulibainisha pia kuwa mazingira ya shule ni hasi kutokana na hali ya kutokuwepo walimu na wataalamu wa kuwashughulikia watoto wa ulemavu huu shuleni.Ili kufikia malengo ya utafiti nadharia ya Utoaji wa Usemi ya Levelt (1989) na nadharia ya Fonolojia Mizani ya Liberman (1975) na Liberman na Prince (1977) zilitumiwa. Nadharia ya utoaji wa usemi ilisaidia kufafanua na kuelezea jinsi michakato na kasoro za usemi na lugha; kwa mfano kigugumizi zinavyotokea. Nadharia ya Fonolojia Mizani iliupa mwongozo utafiti katika uchanganuzi wa viambajengo vya mkazo, toni, mahadhi, tamko na muundo wa silabi jinsi vinavyoathiri usemi wa mfululizo visipotumiwa kisahihi. Shule lengwa zilitembelewa na deta kukusanywa kwa mbinu za uchunzaji na mahojiano. Hojaji na fomu za UChUD7.aji zilitumiwa. Deta iliyopatikana ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa maelezo ya kinathari, majedwali na pia. Utafiti uliweza kubainisha kuwa changamoto nyingi huwakumba sit u wanafunzi wanaogugumiza bali pia walimu na watoto wasiogugumiza. Changaoto hizi zipo katika kila mazingira ya shule, hasa zaidi darasani kwa vile silabasi si pokezi kwa ulemavu hivyo kufanya ujifunzaji kutokuwa kamilifu.