dc.description.abstract | Utafiti huu ulinuia kuchanganua ngeli ya 9/10 (N/N) kwa kutumia kigezo cha uainishaji wa ngeli cha kimofolojia. Ulichunguza kanuni za uingizaji wa nomine nyingi za mkopo na zilizobuniwa ambazo huwekwa katika ngeli hiyo ya 9/10 (N/N). Upatanisho wa kisarufi unaohusiana na ngeli hii ulichunguzwa. Utata unaotokana na upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya 9/10 (N/N) na nomine za ngeli zingine ulichanganuliwa. Kiswahili kama lugha kopaji ilichunguzwa iwapo inatumia ukubaliano wa kisarufi na nomine zilizokopwa au inaelekea kupoteza ukubaliano huo. Data iliyotumika ilipatikana maktabani na nyanjani. Udurusu wa vitabu maktabani, majarida, majuzuu, makala ya makongamano na makala katika mtandao yaliyo na uhusiano na mad a hii ulifanywa kwa kina ili kupata data iliyotumika katika utafiti huu. Mbinu za utafiti zilizotumika nyanjani katika utafiti huu zilikuwa, hojaji, mahojiano na ushiriki. Data ilichanganuliwa kwa kurejelea nadharia zilizoongoza utafiti huu na malengo ya utafiti. Matokeo yaliwasilishwa kupitia katika njia ya maelezo na majedwali. Utafiti huu uliongozwa na nadharia pana ya Utawala na Ufungami iliyoasisiwa na Chomsky mwaka wa 1981. Nadharia ndogo zilizotumika katika utafiti huu na ambazo ziko katika nadharia hii kuu ni nadharia za: Uhusika, X-Baa, Ufungami na Utawala.
Sura ya kwanza ilishughulikia hali iliyochochea mtafiti kuipata mada hii. Malengo na misingi ya nadharia iliyoongoza utafiti huu na yaliyoandikwa kuhusu mada yalifafanuliwa. Mbinu za utafiti zilizotumika katika utafiti huu zilielezwa. Ufafanuzi wa jinsi data ilivyochanganuliwa na jinsi ilivyowasilishwa ulifanywa.
Katika sura ya pili na ya tatu, data iliyokusanywa maktabani ilichanganuliwa. Aina mbalimbali za nomine zilichanganuliwa na uainishaji ngeli kwa kuzingatia kigezo cha kimofolojia na kisintaksia ukafafanuliwa katika sura ya pili. Nomino katika ngeli ya 9/10 (N/N) kwa kutumia kigezo cha kimofolojia zilibainishwa. Upekee wa
ngeli hii ulithibitishwa na upatanisho wa nomine za ngeli hii pamoja na vivumishi na vitenzi ukashughulikiwa katika sura ya tatu.
Katika sura ya nne, data iliyokusanywa nyanjani imechanganuliwa na ikawasilishwa. Mbinu zilizotumiwa kukusanya data zimeelezwa katika utafiti huu.
Sura ya tano imeeleza matokeo, mapendekezo na hitimisho la utafiti huu.
Utafiti huu uligundua kuwa nomine zinazoainishwa katika ngeli ya 9/10 (N/N) ni zile zinazoendelezwa kwa njia sawa katika hali ya umoja na wingi na zilizo na kiambishi awali IN!. Kiambishi awali hiki kina alomofu INYI, IMI na mofu kapa (/0/). Ilitambuliwa kuwa ngeli hii ya 9/10 (N/N) ilikuwa na nomine nyingi za kigeni
na chache zenye asili ya Kibantu. Nomino hizi za kigeni ziliingizwa katika ngeli hii kwa sababu ya kutokuwa na kiambishi awali IMI au !N!.
Vipengele vifuatavyo viliwatatiza wanafunzi wa shule za upili: upatanisho wa kisarufi wa nomina katika ngeli tofauti tofauti, mpangilio wa maneno katika sentensi, uteuzi usiofaa wa msamiati, maendelezo ya maneno na uainishaji wa nomino zingine katika makundi ya ngeli. Athari za ngeli ya 9/10 (N/N) katika nomino za ngeli zingine ilidhihirika. Utafiti uligundua kuwa nomina za ngeli za 7/8 (KINI), 5/6 (JI/MA), na 3/4 (MIMI) zilitumia upatanisho wa kisarufi wa ngeli ya 9/10 (N/N).
Ujumlishaji wa kanuni za ngeli suluhishi ya 9/10 (N/N) katika kazi hii kwa jumla, umethibitisha kuwa lugha ya Kiswahili inaelekea kupoteza upatanisho wake na huenda ikawa inaelekea kubadilika. | en_US |