Show simple item record

dc.contributor.advisorMasinde, E. W.
dc.contributor.advisorPamela Ngugi
dc.contributor.authorKinara, Gladys
dc.date.accessioned2012-07-05T12:40:04Z
dc.date.available2012-07-05T12:40:04Z
dc.date.issued2012-07-05
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/5276
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages: 135p. The PL 8704 .K5M32 2012
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza jinsi riwaya za: Ua la Faraja (2005) na Kala Tufaha (2007) zilivyosawiri usemi unaokusudia kuwapa tumaini walioathiriwa na maradhi ya UKIMWI na kuonya wasio na maradhi haya dhidi ya mienendo inayoweza kuwafanya kuambukizwa. Katika kuchunguza jinsi riwaya hizi zilivyosawiri suala la UKIMWI, utafiti huu umechunguza usemi unaotumiwa kuusawiri UKIMWI, athari ya maradhi haya kwa wahusika katika riwaya husika, na kuonyesha nafasi ya riwaya hizi katika kukabiliana na suala zima la UKIMWI pamoja na changamoto zinazotokea. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Naratolojia pamoja na ya Matendo ya Usemi. Kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia zilizotumiwa, mtafiti alihakiki riwaya zilizoteuliwa ili kupata data iliyotosheleza mahitaji ya utafiti. Data iliyopatikana imerekodiwa na kuchanganuiiwa kulingana na malengo na maswali ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia. Data imewasilishwa kwa maelezo katika utaratibu huu: Sura ya kwanza ya utafiti imetanguliza mada, maswali yanayoongoza utafiti, malengo ya utafiti, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu ya kuchagua mada na misingi ya nadharia. Sura ya pili imechunguza usemi uliotumiwa kusawiri UKIMWI katika riwaya husika. Sura ya tatu imechunguza athari ya maradhi ya UKIMWI kwa wahusika. Sura ya nne imechunguza nafasi ya masimulizi haya katika kukabiliana na suala la UKIMWI na changamoto zake. Utafiti huu pia umedengua maana zilizohusishwa na maradhi ya UKIMWI na kuwapa matumaini wanaougua na walioathiriwa. Tumehitimisha utafiti wetu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo katika sura ya tano. Utafiti huu umekusudiwa kuwafaa wasomi, watafiti, taaluma ya udaktari, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayoshughulika na kukabiliana na suala la UKIMWI na wanajamii kwa jumla.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isoenen_US
dc.subjectMkufya
dc.subjectW. E. Ua la faraja
dc.subjectHistory and criticism
dc.subjectBabu Omar
dc.subjectKala tufaha
dc.subjectAIDS (Disease)
dc.subjectKenya
dc.subjectHIV infections
dc.titleMaudhui ya ukimwi katika ua la faraja na kala tufahaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record