• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Methali za Kiswahili kama chombo cha mawasiliano: mtazamo wa kisiimu - Jamii

Thumbnail
View/Open
Abstract (4.472Kb)
Date
2012-06-06
Author
Maitaria, Joseph N.
Metadata
Show full item record
Abstract
Tasnifu hii imejadili Methali za Kiswahili kama chombo cha mawasiliano. Kazi hii inajaribu kuonyesha kwamba Methali kama vile lugha, ni zao la jamii na hutokana na utamaduni wa jamii mahsusi. Haya yote yamechunguzwa chini ya msingi wa Isimu-Jamii. Katika kutekeleza lengo langu nimegawanya tasnifu hii kwa sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi. Sura hii inaonyesha malengo ya tasnifu hii, sababu za kulichagua somo hili na nadharia ya tasnifu hii. Aidha nimeeleza kazi ambazo zimefanywa kuhusu methali kwa ujumla. Sura ya pili inajadili historia ya Waswahili na utamaduni wao. Imani yangu ni kuwa Waswahili ni jamii yenye makazi yake pwani ya Afrika Mashariki ni uvumi kwamba jamii hii iliibuka baada ya wageni (Waarabu) kuja na kutamakani sehemu hizo. Fauka ya hayo nimeelezea namna methali za Kiswahili huibuka katika mazingira na utamaduni mahsusi. Sura ya tatu nimejadili sifa mbalimbali zinazobainika katika baadhi ya methali za Kiswahili. Sura ya nne imeshughulikia matumizi ya methali za Kiswahili katika mawasiliano ya kijamii. Katika kufanya hivyo inabainika kuwa matumizi ya methali katika mawasiliano huathiriwa na miktadha na utamaduni wa jamii. Sura ya tano ndiyo hitimisho. Nimetoa msimamo wangu kwamba methali kama vile lugha, huibuka katika mazingira maalum. Kwa hivyo matumizi ya methali katika mawasiliano huathiriwa siyo tu na miktadha bali pia na tamaduni zilimoibuka.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4915
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback