Matumizi ya taswira kama kielelezo cha uhalisi katika tenzi wa alinkishafi
Loading...
Date
2012-05-18
Authors
Momanyi, Clara
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii ni uhakiki wa matumizi ya taswira na jinsi mbinu hii ya kifasihi inavyotumiwa na msanii katika kubainisha uhalisi. Kwa hivyo tunachunguza jinsi mshairi Sayyid Abdalla bin Ali bin Nasir anavyotumia taswira katika utenzi wake kudhihirisha uhalisi. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti katika uhakiki wetu ambapo tunazingatia somo la utafiti wetu pamoja na madhumuni, sababu na upepo wa utafiti huu. Halikadhalika, tumegusia yale yaliyoandikwa na wengine kuhusu somo hili pamoja na madhumuni, sababu na upeo wa utafiti huu. Halikadhalika, tumegusia yale yalivyoandikwa na wengine kuhusu somo hili pamoja na machache kuhusu nadharia inayotuongoza katika uchunguzi wetu. Tunatoa pia njia za utafiti wetu ambazo tunawajibika kuzitumia katika kazi hii. Sura ya pili inajadili uhusiano wa matukio ya historia na utenzi wa Al-Inkishafi. Katika sura hii tunajaribu kuonyesha jinsi matukio mbalimbali ya historia yalivyoweza kuchangia katika kuibusha sanaa hii. Matukio ya historia yanayojadiliwa hapa ni yale tu ambayo yamechangia katika uteuzi wa taswikra kama zinavyotumiwa na msanii. Sura ya tatu inazingatia mazingira ya pate na uhusiano wake na utenzi wa Al-Inkishafi. Sura hii tumeigawa katika sehemu kadha, kwa mfano, mazingira ya kijiografia, kijamii, kiuchumi na kisiasa. Sehemu hizi zote zinachangia katika kuonyesha uhusiano uliopo kati yazo na utunzi huu, hasa jinsi ambavyo mshairi anachota taswira zake katika mazingira halisi yaliyomzunguka. Sura ya nne inachunguza uhusiano uliopo kati ya muudo wa kazi uliokuwepo wakati wa mtunzi, na utenzi wake. Halikadhalika, tunachunguza matumizi ya lugha ya wakati wa mtunzi, na uhusiano wake katika utenzi huo. Hapa tunazingatia matumizi ya lugha katika kuibusha taswira hizo na iwapo lugha hiyo ni ile iliyokubalika wakati wa mtunzi. Sura ya tano inajadili kwa undani matumizi ya taswira katika kubainisha uhalisi . Sura hii imegawanywa katika sehemu mbili; sehemu inayojadili taswira za kuonekana, na ile inayojadili taswira za hisi. Hapa tunajadili jinsi mshairi anavyo-tumia taswira katika kutudhihirishia uhalisi kama unavyojitokeza katika utenzi huu. Sura ya sita ni hitimisho la uchunguzi wetu. Katika sura hii, tumetoa muhtasari wa kazi yetu kwa ujumla, yakiwemo matokeo ya uchunguzi huo. Halikadhalika, tumetoa ibara na msamiati mgumu ili kurahisisha ufahamu wa utenzi huu. Picha na ramani tulizotumia zitasaidia pia katika kuelewa zaidi ufafanuzi wetu.
Description
The PL 8704.I5 M6
Keywords
Swahili poetry