Ishara za mawasiliano katika matambiko ya matanga maalum miongoni mwa jamii ya wabukusu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-03-29
Authors
Olunga, Doreen Omito
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unachanganua ishara za mawasiIiano na utumizi wa lugha katika uwasiIishaji wa matambiko ya matanga maalum miongoni mwa jamii ya Wabukusu. Lengo kuu la utafiti huu oi kubainisha namna ambavyo ishara tamkwa na zisizo za kutamkwa pamoja na utumizi wa lugha huweza kuwasilisha maana katika jamii husika kupitia kwa ufasiri wa ishara hizo. Tumechanganua ishara tamkwa na zile zisizotamkwa pamoja na matumizi mbalimbali ya lugha. Utafiti wetu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki na iIe ya Uchanganuzi Amilifu wa Utamaduni. Data ilikusanywa kupitia utafiti wa maktabani na ule wa nyanjani. Maktabani tuliweza kuvisoma vitabu, tasnifu mbalimbali na majarida yanayohusiana na mada yetu ya utafiti. Nyanjani tuliweza kuwa na mahojiano tukiongozwa na maswali ya mahojiano tuliyotunga kabla ya kwenda nyanjani. Tulichanganua data kwa njia ya maelezo. Katika matokeo ya utafiti huu tulibaini kwamba ufasiri wa Ishara Tamkwa, Zisizotamkwa na utumizi wa lugha huweza kuwasilisha maana fulani katikajamii kutegemea muktadha. Kazi hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi unaojadili suala la utafiti, misingi ya nadharia, sababu za kuchagua mada, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, upeo wa utafiti na mbinu za utafiti. Sura ya pili imejadili ishara za mawasiliano na utumizi wa lugha katika uwasilishaji wa matambiko ya matanga ya kawaida iii kuuwekea msingi utafiti wetu. Sura ya tatu nayo imechanganua ishara za mawasiliano na utumizi wa lugha katika uwasiIishaji wa matambiko ya matanga maalum miongoni mwa jamii ya Wabukusu kwa kuzingatia kigezo cha kisababishi cha kifo cha mhusika. Imebainika kuwa uwasilishaji wa matambiko haya hubadilika na pia ishara na lugha huwa tofauti kutegemea kilichosababisha kifo cha mhusika. Sura ya nne nayo imechanganua ishara za mawasiliano na utumizi wa lugha kwa kuegemea kigezo cha hadhi ya mhusika katika jamii. KiIichobainika hapa ni kuwa ishara na lugha hubodilika kwa kuzingatia anayehusika (yaani marehemu), Sura ya mwisho ni hitimisho. Katika sehemu hii tumebaini namna lugha, muktadha na hadhi ya mhusika (marehemu) zinavyoathiri uwasilishaji wa matambiko na jinsi zinavyodokeza ishara na lugha tumikizi. Mazingatio haya yamefanya uwasilishaji wa matambiko kutimiza malengo yake. Katika sura hii pia maelezo yametolewa kwa muhtasari pamoja na matokeo, changamoto na mapendekezo ya utafiti.
Description
The PL 8092 .B87O4
Keywords
Death --Social aspects --Kenya | Funeral rites and ceremonies --Kenya | Kusu (African people) --Kenya | Kusu language --Kenya
Citation