Matatizo ya kisarufi miongoni mwa wanafunzi wa Kikipsigis wanaojifunza Kiswahili sanifu: mtazamo wa lugha kadirifu
Loading...
Date
2012-03-29
Authors
Chepkwony, Leonard Cheruiyot
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Lengo kuu la kazi hii ni kuchunguza matatizo ya kisarufi miongoni mwa wanafunzi wa Kikipsigis wanaojifunza .Kiswahili Sanifu. utafiti huu ulifanywa kwa kutumia. misingi ya nadharia za Lugha Kadirifu na Uchanganuzi Makosa. Nadharia ya Lugha Kadirifu hurejelea maumbo ya muda mfupi ya kisarufi yanayoundwa na wanafunzi wa lugha ya pili wanapojaribu kujifimza lugba hiyo. Nadharia hii huchukulia kuwa, lugba ya mwanafunzi hupitia viwango kadhaa kabla ya kufikia kwenye ukamilifu wa ujuzi wa lugha ya pili. K wa kutumia misingi ya nadharia bizi, tumebaini ehanzo, aina na kiasi eha kutokea kwa makosa ya wanafunzi wa Kikipsigis wanaojifunza Kiswahili Sanifu na kupendekeza mikakati ya ufundishaji inayoweza kutumiwa iIi kupunguza au kuondoa makosa hayo.
Katika utafiti huu, mbinu zifuatazo zilitumiwa kukusanyia data: Hojaji, mahojiano na utazamaji. Majaribio manne yalitumiwa. Jaribio la kwanza lilihusu kutafsiri sentensi za Kikipsigis kwa Kiswahili. Jaribio hili lilijaribu kuehunguza iwapo kuna athari za Kikipsigis katika matumizi ya Kiswahili. Jaribio la pili lilikuwa ni kujaza mapengo yaliyoachwa wazi katika sentensi. Jaribio hili lilifaa iii kudlubiti wanafunzi kwa kuwalazimisha watoe majibu kulingana na matakwa ya mtafiti. Jaribio la tatu lilihusu uandishi wa insha. Wanafunzi walihitajika kuandika insha ya ukurasa mmoja juu ya 'Kijiji ehetu.' Jaribio la mwisho lilihusu kusikiliza na kumngumza. Mwanafunzi alihitajika kusimulia kwa kifupi hadithi anayoipenda huku mtafiti akinasa kwa kanda.
Utafiti huu unahusu ujifunzaji wa lugha ya pili na unapatikana katika taaluma ya Isimu Tumikizi. Tumejikita tu katika matatizo ya kimofolojia na kisintaksia. Sampuli zilitolewa kutoka wilaya ya Bomet. Jumla ya wanafunzi sitini walichunguzwa kutoka shule nne za msingi na Wanafunzi wa darasa la sita, saba na nane walihusika. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa makosa mengi ya kisarufi yanatokana na athari za lugha ya Kikipsigis. Makosa hayo pia yalihusu ujumlishaji mno wa baadhi ya maumbo ya sarufi ya Kiswahili.
Description
Department of Kiswahili and African Languages,142p.The PL 8702 .C48 2011
Keywords
Swahili language --Grammar