Mbinu Ya Ubunilizi wa Kisayansi Katika Riwaya: Bina-Adamu (K. W. Wamitila) na Babu Alipofufuka (S. A. Mohamed)
Loading...
Date
2018-11
Authors
Mucee, Franklin Mukembu
Wafula, Richard Makhanu
King’ei, G. K.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
International Academic Journal of Social Sciences and Education (IAJSSE)
Abstract
Utafiti huu ulihusu mbinu ya Ubunilizi wa
Kisayansi katika mtindo wa riwaya teule za
Bina Adamu K. W. Wamitila (2002) na ile
ya Babu Alipofufuka ya S.A. Mohamed
(2001). Utafiti huu hivyo basi umeonyesha
kwamba sayansi bunilizi ni kipera cha
riwaya kinachopatikana katika fasihi ya
Kiswahili na ambacho kinaendeleza
maudhui ya sayansi na teknolojia katika
utamaduni wa jamii zinazotumia lugha ya
Kiswahili kuwasiliana. Malengo ya utafiti
huu yalijikita katika kubainisha maana ya
sayansi bunilizi na. kudhihirisha sifa za
sayansi bunilizi zinazopatikana katika
riwaya hizi. Vile vile utafiti huu ulilenga
kudhihirisha-kwamba riwaya hizi
zinashughulikia sayansi bunilizi mbali na
kuonyesha mbinu za kimasimulizi
zinazozifanya riwaya za Babu Alipofufuka
na Bina-Adamu kuwa sayansi bunilizi.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya
sayansi bunilizi ambayo imehusishwa na
mawazo yake Jules Verne na H.G. Wells
(1950), nadharia inayoshikilia maudhui ya
sayansi na teknolojia ya wakati uliopo na
wakati ujao, mtindo wa kinjozi ambapo
matukio ya kiajabu yanahusishwa na
usimulizi usioaminika katika misingi ya
uhalisia. Nadharia hii pia haionyeshi mahali
na nyakati, zinaweza kuwa ni zijazo. Aidha
hushughulikia maswala ya athari za sayansi
na teknolojia dhidi ya maadili ya jamii. IIi
kufanikisha utafiti huu data yote
iliyohitajika ilikusanywa kutoka maktabani
ambapo maktaba nyingi zilitembelewa kwa
lengo la kukusanya data iliyohusiana na yale
yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti.
Mtafiti alidurusu yaliyoandikwa kuhusu
sayansi bunilizi katika riwaya teule.
Majarida, majuzuu, tasnifu na machapisho
mengine yanayohusiana na kuafiki mada na
malengo ya utafiti yalipekuliwa. Riwaya
teule ambazo ni Bina-Adamu (2002) na
Babu Alipofufuka (2001) zilisomwa na
kuchambuliwa kwa kina ili kubainisha
malengo ya utafiti yanayozifanya riwaya
hizi kuwa sayansi bunilizi. Data
iliyopatikana kwenye riwaya hizi
ilichanganuliwa kwa kunukuliwa kwenye
daftari kwa kuzingatia malengo ya utafiti
kisha baadaye data hii ikawasilishwa kwa
njia ya mae1ezo yaliyozingatia ufafanuzi wa
sayansi bunilizi kama kipera cha fasihi ya
Kiswahili katika riwaya. Uwasilishaji wa
data ulijifunga katika malengo ya utafiti
pamoja na mihimili ya nadharia teule ya
sayansi bunilizi. Utafiti huu umekuwa na
mchango mkubwa kwa kuwa mada ya
sayansi bunilizi katika fasihi ya Kiswahili
imebainisha uwiano kati ya maendeleo ya
sayansi na teknolojia na sayansi bunilizi ya
Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki.
Kwa kuwa sayansi bunilizi huzungumzia
mambo ya kiajabu na mapya, imeweza
kuzua msamiati mpya ambao utaingizwa
katika lugha ya Kiswahili na hivyo kupanua
msamiati wa lugha ya Kiswahili kwa jumla.
Huu ni mchango chanya kwani lugha ya
Kiswahili ingali inakua.
Description
Article
Keywords
mbinu ya ubunilizi, kisayansi, riwaya, Bina-Adamu, K. W. Wamitila, Babu Alipofufuka, S. A. Mohamed
Citation
Mucee, F. M., King’ei, G. K., & Wafula, R. M. (2018). Mbinu ya ubunilizi wa kisayansi katika riwaya: Bina-Adamu (KW Wamitila) na Babu Alipofufuka (SA Mohamed). International Academic Journal of Social Sciences and Education, 1, 1-38.