Usemezano katika tamthilia ya Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-01-31
Authors
Jessee, Murithi Joseph
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Katika tasnifu hii tumechunguza usemezano katika tamthilia ya Kiswahili. Tumetumia tamthilia tatu ambazo ni Mashetano, (Hussein, 1971), Kilio cha Haki, (Mazrui, 1981) na Amezidi, (mohammed 1995) kubainisha kuwa usemezano upo katika tamthilia ya Kiswahili. Malengo ya utafiti yamekuwa ni kuchanguza kama kuna usemezano katika tamthilia ya Kiswahili, kuonyesha usemezano huu umewasilishwa kwa namna gani, na kutanua nadharia ya usemezano kwa kuitumia kuchunguza usemezano. Ilibainika kwamba usemezano upo katika tamthilia ya Kiswahili. Sifa za usemezano ambazo zilizingatiwa na kudhahirishwa ni sajili mbalimbali, uhusiano na athari za matini zingine, mtagusano baina, ya "mimi" na "yeye", masimulizi ya moja kwa ya kifasihi kutoka kwa mwandishi, na uzungumzi nafsia wa wahusika kupitia kwa lugha ya wahusika. Sura ya kwanza, ambayo ni utangulizi imeshughulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua mada madhumuni ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili, tumejadili usemezano katika tamthilia ya Mashetani. Imedhihirika kwamba tamthilia hii ni mkusanyiko wa sajili mbalimbali, ina masimulizi ya kifasihi ya moja kwa moja kutoka kwa mwandishi, inahusiana na kuathiriana na matini zingine kama vile matini za dini, kifasihi, kihistoria na kadhalika. Pia kuna mtagusano baina ya nafsi ya "mimi" na "yeye", ina uzungumzi nafsia wa wahusika kupitia kwa lugha waliopewa. Aidha, lugha waliopewa wahusika ilidhihirika kuwa inaakisi malengo na majukumu waliopewa kuyatekeleza. Sifa hizi pia zinajitokeza katika tamthilia za Kilio Cha Haki na Amezidi. Tamthilia hizi zimejadiliwa katika sura ya tatu na nne. Sura ya tano ambayo ni ya mwisho inaonyesha hitimisho na matokeo ya utafiti kwa ujumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine ambao unaweza kufanywa katika uwanja huu pia yametolewa. Kutokana na kazi hii ni dhahiri kuwa nadharia ya usemezano inaweza kutumiwa kwa mafanikio makubwa katika uhakii wa tamthilia ya Kiswahili.
Description
The PL 8704.J4U9
Keywords
Swahili literature--History and Criticism//Mohammed, S.A.--Amezidi--History and criticism//Mazrui,A.--Kilio cha haki--History and Criticism//Hussein,E.N.--Mashetani--History and Criticism
Citation