Ubunifu wa mtafsiri: Tamthilia ya masaibu ya ndugu jero
Loading...
Date
2011-12-30
Authors
Muigai, Mary Njambi
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu unahusu ubunifu wa mtafsiri katika kazi za kifasihi. Lengo la utafiti huu ni kubainisha ni kwa kiasi gani ubunifu wa mtafsiri umedhihirika katika tamthilia tafsiri ya Masaibu ya Ndugu Jero. Nadharia ya ufasiri ndio iliyotumiwa kuutathmini ubunifu wa mtafsiri katika tamthilia tafsiri ya Masaibu ya Ndugu Jero. Kwa kuzingatia misingi ya nadharia hii, dhana zinazohusiana na utamaduni wa kidini na vifaa pamoja na tamathali za usemi zimetathminiwa. Aidha, utafiti huu umenuia kuchunguza iwapo ubunifu wa mtafsiri umechangia katika kuimarisha ufahamu na kuendeleza maudhui na dhamira ya mwandishi wa matini chasili kwa wasomaji wa matini tafsiri.
Tasnifu hii imegawika katika sura tano. Sura ya kwanza, ambayo ni utangulizi wa Tasnifu, inashughulikia swala la utafiti pamoja na madhumuni, sababu na upeo wa utafiti. Kadhalika, kuna maelezo kuhusu yale yaliyoandikwa " na wengine kuhusu mada hii, mbinu za utafiti na nadharia iliyoongoza utafiti huu.
Sura ya pili, tatu na nne ni uchanganuzi wa data uliojikita katika dhana zinazohusiana na utamaduni wa kidini na vifaa pamoja na matumizi ya tamathali za usemi.
Sura ya tano ni hitimisho la utafiti. Katika sura hii kuna muhtasari pamoja na matokeo ya utafiti kwa ujumla. Mapendekezo ya utafiti mwingine unaoweza kufanywa katika uwanja huu pia yameonyeshwa.
Description
The PL 8704.U32M8
Keywords
Swahili litarature--Study and teaching//Masaibu ya ndugu Jero