Usa Wazishaji wa usemi kati ya waasia na waafrika katikati mwa jiji la Nairobi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-28
Authors
Kitonga, Nelly Nzula
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu wa isimujamii unachunguza usawazishaji wa usemi kati ya Waasia na Waafrika katikati mwa jiji la Nairobi. Unajikita katika maingiliano ya kikazi pale ambapo Waasia ni waajiri na Waafrika ni wafanyakazi na wateja katika maduka ya Waasia hao. Lengo la uchunguzi huu ni kubainisha namna ya usawazishaji wa usemi kati ya Waasia na Waafrika, kuchunguza, kutambua na kueleza viwango vya kiisimu hasa vya kisemantiki na kisintaksia vinavyobadilishwa wakati wa utaratibu wa usawazishaji wa usemi. Aidha utafiti huu unanuia kufafanua sababu zinazowamotisha Waafrika na Waasia kubadilisha usemi wakati wa maingiliano ya ana kwa ana. Waafrika na Waasia walibadilisha mtindo wa usemi ili kuonyesha mwingiano na ujitengaji. Mwingiano na ujitengaji kiusemi ulisababishwa na uchaguzi wa lugha wa kipekee, uchaguzi wa lugha usio wa kipekee na uchaguzi wa lugha wa kubahatisha, na uzingativu wa muundo wa sentensi. Wazungumzaji wanaonyesha mwingiano iwapo wanatafuta kukubalika, kueleweka, kuwa sawa na wasikilizaji, kupunguza gharama kiusemi na kuzidisha manufaa yanayotarajiwa. Watajitenga kiusemi kama njia ya kujitambulisha kijamii, kuonyesha kutokubaliana na mada ya mazungumzo na pia kutaka kuwa tofauti na wasikilizaji. Kazi yote iligawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni usuli wa utafiti, swala la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili inafafanua msingi wa nadharia, launi ya Kiswahili ya Waasia na lugha ya Kiswahili. Katika sura ya tatu, usawazishaji wa usemi katika kiwango cha semantiki umefafanuliwa pamoja na uhusiano wake na nadharia za Upekee na Usawazishaji Usemi. Sura ya nne inatoa maelezo ya namna inavyokuwa wakati Waasia na Waafrika wanapojisawazisha kiusemi katika kiwango cha sintaksia kwa msingi wa nadharia za Sarufi Miundo Virai, Upekee na Usawazishaji Usemi. Mwisho, sura ya tano inahusu muhtasari, matokeo, mahitimisho na mapendekezo yanayojitokeza katika utafiti. Kupitia nadharia ya usawazishaji Usemi na nadharia ya Upekee utafiti huu umebaini kwamba Waasia na Waafrika wanabadili lugha kwa sababu za kiuchumi na kisaikolojia.
Description
The PL 8701.K5
Keywords
Swahili language--Kenyan Asians//Swahili language--Kenyans//Swahili language--Nairobi city
Citation