• English
    • français
  • English 
    • English
    • français
  • Login
View Item 
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
  •   Repository Home
  • Master Theses and Dissertations(MST)
  • MST-School of Humanities and Social Sciences
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages
  • View Item
JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

Maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora

Thumbnail
View/Open
Full Text Thesis (61.70Mb)
Date
2008-04
Author
Ochenja, Rajab
Metadata
Show full item record
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia maigizo kama mbinu ya maudhui katika riwaya mbili za Ken Walibora. Riwaya zilizoshughulikwa ni Ndoto ya Amerika, (2001) na Kufa Kuzikana, (2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto za uhalisia na uigizaji. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu hasa ikizingatiwa ya kwamba riwaya zilizotafitiwa zimesheheni matukio mengi ambayo yanaakisi mambo yanayotokea katika maisha ya kawaida. Kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa riwaya za Walibora zilizotafitiwa zina sifa za kitamthilia. Mwandishi ametumia mbinu mahsusi za maigizo ambazo zimezifanya riwaya hizi kubainika kama tamthilia. Kwanza, mwandishi amewashirikisha wahusika wake zaidi katika kutenda na kusema, kuliko kusema pekee. Vitendo vyao vimeandamana na mazungumzo. Haya yanaonekana kupitia wahusika kama Isaya, Madoa na 'Rock Mwamba' au Zablon Okutoyi katika Ndoto ya Amerika (2001); na Akida, Tim na Tamari katika Kufa Kuzikana (2003). Utafiti pia umebainisha kuwa katika kuzifanya riwaya zake zibainike kama tamthilia, Walibora amewafanya wahusika wake wote kuwa binadamu halisi wanaowasiliana moja kwa moja. Jambo hili limeyapa masimulizi yake uhai na uhalisi zaidi kiasi cha kuonekana kama maigizo. Katika matukio mengi, mwandishi amewafanya wahusika wake wawasiliane wakitumia wakati uliopo, jambo ambalo linatoa taswira ya uigizaji. Kupitia utafiti, imebainika pia kuwa riwaya za Walibora zilizotafitiwa zimebeba wahusika wa kila umri na jinsia; hili ni jambo la kawaida katika maisha halisi kwa sababu linaakisi hali inayopatikana katika maisha ya kila siku; na maisha ni maigizo. Utafiti pia umebainisha kuwa mwandishi ametumia mabadiliko ya mandhari katika riwaya zilizohakikiwa ili kujenga taswira ya uigizaji. Mandhari yamebadilishwa ili kuafiki mada iliyohusishwa katika mazungurnzo baina ya wahusika. Kupitia riwaya hizi, kuna mandhari ya shule, ofisi, mahakama, sokoni na hata kituo cha polisi. Hili ni sawa na jukwaa ambalo hupatikana katika maigizo. Kubadilika kwa mandhari kila mara kunaweza kukamithilishwa na mabadiliko yanayotokea jukwaani katika michezo ya kuigiza ili kuashiria kumalizika kwa onyesho moja na kuanza kwa onyesho lingine. Utafiti umebainisha vile vile kuwa maudhui yanayoshughulikiwa katika kazi za Walibora yamechangia pakubwa kuzifanya zikaonekana kama maigizo. Maudhui ya uhalifu, ukabila, ubinafsi na ukatili yamewasilishwa kwa hadhira kupitia maigizo ya moja kwa moja ya wahusika mbalimbali. Utafiti huu utakuwa na mchango ufuatao; kwanza, umetuonyesha kuwa inafaa tuwe na mtazamo tofauti na vigezo vingine vya kuzihakiki riwaya badala ya kuselelea katika mitazamo ya kijadi iliyokuwa ikichukulia riwaya kama utanzu mahsusi unaojitosheleza. Kupitia utafiti hull, imebainika kuwa riwaya za WaIibora zilizotafitiwa zina pia sifa za kitamthilia. Mchango mwmgme ni kuwa, baada ya utafiti, imebainika kuwa riwaya yoyote inaweza pia ikawa na sifa za kitamthilia kama ilivyobainika katika riwaya za Walibora zilizotafitiwa. Utafiti huu pia ni miongoni mwa kazi chache ambazo zimewahi kuhakiki baadhi ya kazi za Walibora kwa mtazamo tofauti. Kazi hizo zimehakikiwa kama zinazobeba sifa mseto za tanzu mbaIimbali na kutofautiana na mitazamo ya awali iliyochukulia tanzu tofauti za fasihi andishi kama zinazojitosheleza. Kwa hivyo, utafiti huu utawapatia wasomi wengine wa kazi za fasihi ya Kiswahili barabara tofauti za kufuata wakiwa katika safari ya kusaka mengi zaidi katika taaluma hii.
URI
http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/19497
Collections
  • MST-Department of Kiswahili and African Languages [234]

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback

 

 

Browse

All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

My Account

LoginRegister

Designed by Library ICT Team copyright © 2017 
Contact Us | Send Feedback