Usimulizi katika Riwaya ya Dharau ya Ini
Loading...
Date
2018-10
Authors
Wambui, Janet
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti ulichunguza usimulizi katika riwaya ya Dharau ya Ini (2007) ya Kyalo Wamitila. Malengo ya utafiti yalikuwa ni kubainisha sauti za usimuliaji na viwango vya usimulizi katika riwaya; kuonyesha nafasi ya wakati katika usimulizi na kudhihirisha uwasilishaji wa usemi na fikra za wahusika katika uendelezaji wa hadithi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya naratolojia kwa kuzingatia mwelekeo wa Gennette (1980). Naratolojia ilitumika katika kuchunguza sifa za muundo wa simulizi kwa kugawa vipengele vyake na kuzingatia uamilifu na uhusiano uliopo. Mihimili ya nadharia hii imesaidia katika kuihakiki matini kwa kuchunguza mbinu za usimulizi zinazotumika katika uendelezaji wa hadithi. Utafiti ulijikita maktabani ambapo vitabu, tasnifu na majarida yaliyoangazia masuala ya nadharia na usimulizi yalisomwa. Mbinu ya sampuli ya kimaksudi ilitumika katika ukusanyaji wa data iliyotokana na usomaji wa riwaya ya Dharau ya Ini. Mafungu yanayoonyesha sifa za sauti na viwango mbalimbali vya usimulizi, wakati katika usimulizi na uwasilishaji wa usemi na fikra za wahusika yalidondolewa kutoka kwenye matini. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo kulingana na malengo ya utafiti. Utafiti ulibainisha kuwa riwaya imehusisha msimulizi anayeshiriki kama mhusika katika matukio anayosimulia na katika sehemu zingine anasimulia hadithi akiwa nje ya matukio hayo. Riwaya imehusisha matumizi ya mbinu rejeshi na elekezi katika uwasilishaji wa matukio. Ilitambulika kuwa uwasilishaji wa usemi na fikra za wahusika ni njia muhimu ya kubadili mitazamo ya usimulizi katika uendelezaji wa hadithi. Utafiti umetoa mchango kwa kuonyesha jinsi nyingine ya kuchanganua riwaya kwa kuhusisha nadharia ya naratolojia. Mapendekezo yaliyotolewa ni kuwa tafiti zaidi zifanywe ili kuchunguza mbinu za usimulizi katika tungo zingine za fasihi ili kuikuza kazi ya fasihi andishi.
Description
Tasnifu Hii Imewasilishwa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Oktoba 2018