Ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa shule za msingi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017
Authors
Odhiambo, Dorothy Akinyi
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulinuia kuchunguza ufasiri wa ngano za kifantasia miongoni mwa watoto wa darasa la tatu katika shule za msingi nchini Kenya. Lengo kuu lilikuwa kubainisha jinsi watoto wanavyofasiri maudhui, wahusika na mandhari yanayotokana na ngano teule za kifantasia. Vitabu vilivyosomwa na kufasiriwa ni: Kuku na Mwewe (Mpesha, 1998) Paka na Panya (Nyakeri, 2006), Afanyaye Ubaya Hulipwa (Yahya, 2003) na Safari ya Mbinguni (Waihiga, 2006). Kazi hii iliongozwa na nadharia mbili ambazo zilichangiana katika kufanikisha madhumuni. Nadharia hizo ni Mwitikio wa Msomaji na Uhalisiajabu. Utafiti ulifanyika maktabani, mtandaoni na nyanjani. Utafiti huu ulifanywa katika manisapaa ya Homabay. Shule moja ya kibinafsi nay engine ya uma ziliteuliwa kwa kutumia mbinu bahatishi. Watoto walishirikishwa katika kusoma ngano teule katika vikao. Aidha, mtafiti aliandaa majadiliano na watoto huku wakijibu maswali walioulizwa. Data zilizokusanywa zilichanganuliwa kulingana na madhumuni ya utafiti na mihimili ya nadharia. Data zote zimewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili, mtafiti ameandika muhtasari wa ngano zilizoteuliwa. Pia, ufasiri wa maudhui katika ngano hizi umeshughulikiwa. Katika sura ya tatu, ufasiri wa wahusika umejadiliwa. Sura ya nne imeshughulikia ufasiri wa mandhari yanayojitokeza katika ngano zilizosomwa. Sura ya mwisho ni muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Utafiti huu umechangia katika taaluma ya fasihi ya watoto. Washikadau watakaonufaika kutokana nayo ni kama wahakiki, wakufunzi vyuoni, wachapishaji, wazazi, waandishi na miongoni mwa wengine.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili chuo kikuu cha kenyatta. 2017
Keywords
Citation