Mchango wa msimilishaji simulizi katika maonyesho ya filamu: mfano wa Dj. Afro

Loading...
Thumbnail Image
Date
2017-09
Authors
Gathogo, Ephraim Muiga
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa msimilishaji simulizi katika maonyesho ya filamu kwa kurejelea filamu mbili za Kimarekani ambazo ni; Human Time Bomb na Mercenaries. Utafiti ulinuia kuchunguza namna msimilishaji simulizi anavyochangia maudhui katika filamu. Utafiti pia ulilenga kuchunguza mbinu za lugha anazotumia msimilishaji simulizi. Kwa kufanya hivyo utafiti ungebaini jinsi msimilishaji simulizi husawiri wahusika asilia wa filamu. Nadharia iliyotumika kama dira ya utafiti huu ni Naratolojia. Mwanafalsafa wa Kiyunani Plato ndiye mwasisi wa Naratolojia. Baadaye iliendelezwa na wanadharia kama Gennette, Mieke Bal, Stanzel na Manfred Jahn. Naratolojia kama nadharia ya kifasihi hubaini sifa za simulizi na jinsi hutambulika katika muktadha maalum. Naratolojia ilikuwa na nafasi muhimu kuongoza utafiti huu kwa kuwa utafiti wenyewe ulihusisha Msimilishaji simulizi. Mtafiti alitazama na kusikiliza kwa makini usimuliaji katika filamu mbili za DJ Afro na kuchanganua vipengele vya usimulizi alivyotumia msimilishaji simulizi. Mchango wa utafiti huu unahusu dhima ya Msimilishaji simulizi katika kuelewa maudhui na mtindo wa filamu. Utafiti vilevile unaonyesha jinsi lugha ya Kiswahili inavyotumika katika mawanda ya kimataifa.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Septemba 2017
Keywords
Citation