Show simple item record

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOkemwa, Milkah Kerubo
dc.date.accessioned2018-09-19T08:12:26Z
dc.date.available2018-09-19T08:12:26Z
dc.date.issued2017-09
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18618
dc.descriptionTasnifu ya utafiti iliyowasilishwa kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Septemba, 2017en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulitathmini mchango wa fasihi simulizi katika fasihi andishi. Utafiti ulilenga kubainisha umuhimu wa visasili katika utunzi wa riwaya ya Kiswahili. Malengo ya utafiti yalikuwa ni kuonyesha ubainikaji wa visasili, mchango na umuhimu wake katika utunzi wa riwaya ya Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Riwaya hizi ziliandikwa na Katama Mkangi. Utafiti uliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na mwananadharia Kristeva (1966). Kuingiliana kwa matini katika kazi ya fasihi kuna maana ya kazi moja ya kifasihi kuwa na sifa za tanzu nyingine ndani yake ili kupitisha ujumbe. Visasili viliteuliwa kimakusudi kwa mujibu wa malengo ya utafiti. Utafiti ulifanywa maktabani kwa kusoma vitabu viteule kwa kina, miswada, majarida, tasnifu na makala mbalimbali yenye data iliyohusu mada hii. Mtafiti pia alizingatia matumizi ya mtandao ili kupata ujumbe zaidi. Ukusanyaji wa data ulifanywa kwa kuongozwa na nadharia ya utafiti. Aidha, data ilichanganuliwa kwa kuainishwa kwa misingi ya ubainishaji wa visasili, mchango na umuhimu wake. Kisha, uchanganuzi wa data uliongozwa na maswali ya utafiti, malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo na kwa kutoa mifano mwafaka ya aina za visasili katika riwaya teule.Tunatumai kwamba kazi hii itatoa mchango maalum kwa wanafunzi, walimu, wahakiki wa fasihi, wasomi pamoja na wakuza mitaala kwa kuwapa mwanga zaidi kuhusu mchango wa fasihi simulizi katika kukuza na kuendeleza uhakiki wa riwaya teule. Kadhalika, unaangazia suala la kuchanganua visasili kama kipengele cha mwingilianomatini katika ufundishaji na ujifunzaji wa riwaya.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleMchango wa fasihi simulizi katika fasihi andishi: mfano wa visasili katika Mafuta (1984) na Walenisi (1995)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record