Matumizi ya Ushairi katika Tamthilia ya Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-02
Authors
James, W. S.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umechunguza matumizi ya ushairi katika tamthilia ya Kiswahili. Uchunguzi umejiegemeza katika tamthilia tatu za Kiswahili: Mama ee (1987), Kilio cha Haki (1981) na Amezidi (1995). Malengo ya tasnifu hii yalikuwa kuchunguza umuhimu wa ushairi katika kuendeleza utanzu wa tamthilia ya Kiswahili. Aidha kudhihirisha jinsi ushairi ulivyotumiwa kusawiri ujumbe, lugha na wahusika katika tamthilia ya Kiswahili. Hatimaye kuonyesha kwamba ushairi ni mojawapo ya mbinu zinazotumiwa na watunzi wa tamthilia kama mbinu ya kimtindo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya utanzu (Genre theon,) ambayo inaeleweka kama kiainishi cha kundi aina, namna au mtindo wa utendaji wenye kuwasiliana. Kuainishwa na kujulikana kuwa mall ya kundi husika hutokana na sifa bainifu za umbo lake na kuendelezwa kwake. Warasmi kama Aristotle wanasema kwamba tanzu za fasihi zilikuwa tatu to yaani shairi la hisia, drama na tendi. Tanzu hizi zilikuwa na ukuruba mkubwa mno. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia swala la utafiti sababu za kuichagua mada, upeo wa utafiti, madhumuni va utafiti. msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pill imejadili matumizi ya ushairi katika usawiri Nva ujumbe na matumizi ya lugha ya Kishairi katika tamthilia hizo tatu. Sum ya nne, mtafiti amejadili umuhimu wa ushairi katika kusawiri wahusika katika tamthilia. Utafiti ulifanywa kwa kutazama jinsi ushairi ulivyotumiwa na wahusika hao kuendeleza madhumuni ya mchezo. Sura ya tano ni hitimisho. Mtafiti ametoa mulitasari, matokeo kUIlusll utafiti na mapendekezo ya utafiti zaidi
Description
Department of Kiswahili and African Languages, 153p. 2007
Keywords
Mwachofi, ari katini.mama ee--History and criticism//Mazrui, A. Kilio cha haki--History and criticism//Mohammed, S.A. Amezidi--History and criticism//Swahili literature--History and criticism
Citation