Matumizi ya taswira na ukinzano kama kichocheo cha zinduko katika riwaya za G.K.Mkangi (1984) na walenisi (1995)
Loading...
Date
2011-11-16
Authors
Musembi, Naomi N.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umechunguza taswira na ukinzano kama kichocheo cha zinduko katika riwaya za Mafuta (1984) na Walenisi (1995) kwa kutumia nadharia ya uyakinifu wa kijamaa na nadharia ya kimtindo. Kazi hii imechanganua taswira za kuonekana na za hisi zilizotumiwa na Mkangi ili kubainisha maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyojikita katika taswira hizo. Mkangi alilenga kuwazindua wasomaji wake kuhusu hali halisi ya maisha yao na wakati huo huo kuwatolea suluhu la kurekebisha hali hizo.
Utafiti huu una sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi unaojadili suala la utafiti, sababu za kuchagua mada hii, mbinu za utafiti, mapitio ya kazi muhimu na misingi ya nadharia.
Sura ya pili imejadili historia ya mwandishi na mchango wa mazingira yake katika matumizi ya taswira na mbinu ya ukinzano. Pia, aina za taswira zinazopatikana katika mazingira ya mwandishi zimefafanuliwa. Sura ya tatu na nne zimechanganua taswira zinazopatikana katika riwaya za Mafuta na Walenisi.
Sura ya tano ni hitimisho na matokeo ya utafiti ambamo imedhihirika kwamba, Mkangi alitumia mbinu za taswira na ukinzano akiwa na lengo la kumzindua msomaji ili cone uhalisi katika maisha yake.
Kutokana na kazi hii, ni dhahiri kuwa Mkangi alilenga kumzindua msomaji kuhusu athari za utabaka, ubepari, unafiki wa viongozi sheria na nafasi yake katika jamii, umuhimu wa utu na usawa, umuhimu wa mapinduzi katika ujenzi wa jamii mpya, elimu na utafiti, chango wa vijana katika ujenzi wa taifa miongoni mwa mengine. Aidha, imetambulika kwamba, Mkangi alitumia taswira za kuonekana na za hisi kutokana na sababu kwamba, taswira hizi huiwezesa picha kuganda vizuri akilini mwa msomaji ili aupate aupate ujumbe wa mwandishi vizuri. Licha ya hayo, mbinu ya ukinzano imetumiwa kwa ufundi mkubwa i1i kulinganisha hali mbili kinyume ili kumzindua msomaji aone uhalisi katika maisha yake.
Description
The PL 8704.M8M32
Keywords
Mkangi, G.K. Mafuta(1984)--History and criticism//Mkangi,G.K.Walensi (1995)--History and criticism//Kiswahili Literature--History and criticism