dc.description.abstract | Utafiti huu umeshugulikia swala la nadharia kama mkakati wa kufahamu riwaya za Babu Alipofufuka, Bina-Adamu! na mkusanyiko wa hadithi fupi Sadiki Ukipenda. Nadharia iliyotumiwa katika utafiti huu ni ile ya usemezano. Hii ni kwa sababu lengo letu kuu ni kuchanganua jinsi usemezano unavyoweza kujaliza mapengo yanayojitokeza katika riwaya za Babu Alipofufuka, Bina-Adamu! na mkusanyiko wa hadithi fupi Sadiki Ukipenda. Utafiti huu umejaribu kujaliza mapengo yanayoleta matatizo ya ufahamu na usadikifu kazi tulizo teua za kihalisiajabu. Katika kazi hizi matukio yanasawiriwa kiajabu ajabu, ni ya kuogofya, kutisha na hayaeleweki kwa urahisi. Kwa kutumia nadharia ya usemezano, tumerahisisha uelewa na usadikifu wa vipengele hivi.
Tasnifu hii ina sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa tumeshughulikia mada ya utafiti, sababu ya kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu hii mada. Aidha, tumejadili upeo wa utafiti huu na misingi ya nadharia hii iliyouongoza. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa.
Sura ya pili imejadili historia fupi ya uandishi wa waandishi Said Ahmed Mohamed na K. W. Wamitila. Tumeonyesha jinsi walivyobadilisha mtindo wa uandishi wao kutoka kwenye uhalisia hadi kufikia uhalisiajabu. Utafiti umedhamiria kuonyesha jinsi walivyobadili uandishi wao na umuhimu wa kufanya hivyo ili kuonyesha hoja zao kwa uwazi zaidi katika hali zinazobadilikabadilika.
Sura ya tatu inachunguza jinsi nadharia ya usemezano inavyoweza kutumiwa ili kurahisisha uelewa na usadikifu wa vipengele vya kihalisiajabu vinavyopatikana katika riwaya ya Bina-Adamu! na mkusanyiko wa hadithi fupi Sadiki Ukipenda. Mihimili ya nadharia ya usemezano tuliyoitumia ni pamoja na uwili wa usemi, mwingiliano matini, sauti na maana ya neno, kutegemea historia ya lugha na hali tofauti za wakati huo wa kihistoria.
Sura ya nne inachunguza usemezano katika riwaya ya Babu Alipofufuka imeainisha vipengele mbalimbali vya kihalisiajabu na jinsi usemezano unavyoweza kutumiwa kurahisisha uelewa na usadikifu katika vipengele hivi. Vile vile tumehitimisha kwa kuangalia matokeo ya utafiti, matatizo yaliyokabili utafiti na mapendekezo ya utafiti huu.
Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba kuna matatizo ya ufahamu na usadikifu katika kazi nilizoshughulikia. Utafiti pia umethibitisha kwamba kwa kutumia usemezano nimeweza kusahihisha baadhi ya matatizo ya ufahamu na usadikifu. Pia umeonyesha kwamba Said Ahmed Mohamed na K.W. Wamitila wametumia mtindo wa uhalisiajabu ili kueleza matatizo na shida zinazoibuka katika ulimwengu wa sasa ambapo duma ma chukuliwa kama kijiji kimoja.
Kwa kusemezana na matini nje ya riwaya hizi, kazi zingine na fasihi zilizoko katika ujirani wake tumeweza kupunguza uelewa na usadikifu wa matatizo haya na kuyaweka wazi. Kwa kuelewa matatizo haya Waafrika watajibidiisha kuchukua nafasi yao katikati
mwa kijiji na kukoma kukaa pembeni wakiogopa katikati mwa kijiji (Waafrika wanadanganywa na watu wa nchi za kimagharibi kwamba wao (wazungu) tu, ndio wanaweza kuwatatulia matatizo yao na wao wanajitenga kando na kungoja yatatuliwe). | en_US |
dc.subject | Mohamed,S.A.,Babu alipofufuka(2001) -- History and criticism//Wamitila,K.W.,Bina-Adamu!(2002) -- History and criticism//Mohamed,S.A.,Sadiki ukipenda(2002) -- History and criticism//Swahili literature -- History and criticism | en_US |