Matumizi ya methali katika insha za wanafunzi wa shule za msingi wilayani Thika

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-11-14
Authors
Gaitho, Anthony Gitau
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Madhumuni ya kazi hii ni kuchunguza jinsi ambavyo wanafunzi wa darasa la saba hutumia methali katika uandishi wao wa insha. Aidha makosa yanayojitokeza wakati methali zinapotumika yameshughulikiwa pamoja na chanzo cha makosa yenyewe. Chini ya msingi wa nadharia ya Isimu Amilifu, matumizi ya methali katika insha yalichunguzwa kwa kuwashirikisha wanafunzi wa shule za msingi katika wilaya ya Thika (Kenya). Kazi hii imegawanyika katika sura tano. Sura ya kwanza inatoa utangulizi wa kazi yote. Mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, misingi ya nadharia, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusiana na mada ya utafiti pamoja na mbinu za utafiti, yote yameshughulikiwa hapa. Sura ya pili imejadili nafasi ya methali katika insha ambapo maana, muundo, sifa bainifu na dhima ya methali zimejadiliwa. Vile vile methali zimeainishwa kwa mujibu wa utenda kazi wake. Imejitokeza hapa kuwa methali zina uwezo wa kuambatanishwa na tamathali tofauti tofauti za usemi. Aidha sura hii imeshughuldcia aina za insha na sifa za insha bora. Katika sura ya tatu data imewasilishwa na hoja muhimu kujadiliwa. Hapa matumizi ya methali katika insha yarnefafanuliwa. Makosa yaliyojitokeza katika matumizi ya methali yamechanganuliwa kwa mujibu wa aina yake kama vile: kutojua maana ya methali, kubadilisha muundo wa methali, uchopekaji, uziada wa matumizi ya methali miongoni mwa makosa mengine. Nayo sura ya nne imetengewa chanzo cha matumizi yasiyofaa ya methali katika insha. Baadhi ya mambo yaliyoonekana kusababisha makosa haya ni kama vile mwelekeo fmyu wa methali miongoni mwa wanafunzi, athari ya L1, kutojua maana ya methali, kutojua mipaka ya sheria, msisitizo wa walimu na hata vitabu vya kiada ambavyo hutegemewa na wanafunzi na walimu kufunzia lugha ya Kiswahili. Sura ya tano inahitimisha kazi hii kwa njia ya muhtasari. Matokeo ya utafiti huu yakiambatanishwa na mapendekezo yameangaziwa. Jambo lililo wazi ni kuwa wanafunzi wengi hutumia methali katika insha zao. Wakati huo huo, wao hufanya makosa mbalimbali. Hivyo walimu na wakuza mitaala wapaswa kuchukua tahadhari ili kuyakabili makosa yanayojitokeza methali zinapotumika. Hii ni kwa sababu methali ni kipengele muhimu na kinachopendelewa na wanafunzi wanapoandika insha.
Description
Department of Kiswahili and African Languages,107p.The PL 8702.G3M3 2008.
Keywords
Kiswahili language--Composition and excercise, Proverbs, Swahili--Thika--Kenya
Citation