Repository logo
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
Repository logo
  • Communities & Collections
  • All of DSpace
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Mukonambi, Kekonen Stanley"

Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-08) Mukonambi, Kekonen Stanley; Kaui,Titus
    Makala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake The Republic na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la The Poetics na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa YouTube ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Wakaa, Uwasilishaji Usemi na Wahusika katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya
    (Kenyatta University, 2025-11) Mukonambi, Kekonen Stanley; King'ei, Kitula Osore, Miriam
    Utafiti huu ulichunguza wakaa, uwasilishaji usemi na wahusika katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutumia hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo ya mbinu hizi za kimtindo ni usimulizi. Utafiti huu ulichunguza vipengele vya usimulizi; wakaa, uwasilishaji wa usemi na wahusika. Wakaa ni mpangilio wa matukio katika hadithi. Uwasilishaji wa usemi ni namna ambavyo maana hutolewa kwa kutumia lugha ilhali wahusika ni viumbe wa kisanaa wanaoendeleza kazi ya kifasihi. Malengo ya utafiti huu ni: kubainisha vipengee vya wakaa, uwasilishaji wa usemi na wahusika katika hotuba teule na kujadili dhima ya wakaa, uwasilishaji usemi na wahusika katika hotuba teule. Nadharia iliyotumika ni ya Naratolojia kwa kuzingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Mtazamo wake ni wazi kwani huwasaidia wasomaji kutofautisha kwa urahisi viwango vya masimulizi na kuchanganua matini kwa hatua. Aidha, haujatumika na tafiti nyingi ikilinganishwa na ule wa Gerald Genette. Mihimili yake ilifaa kwani iliweka wazi vipengele ambavyo vilishughulikiwa na kutathmini nafasi yavyo katika uelewekaji wa hotuba teule. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumika kuteua hotuba teule za Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wa chama cha TNA na JP, Mhes. Raila Odinga wa chama cha ODM na Rais Dkt. William Ruto wa chama cha URP, JP na UDA zilizotolewa kati ya mwaka 2013 hadi 2023. Utafiti ulifanyika maktabani ambako data ilikusanywa kwa njia za usomaji makini kwa kupitia makala, nyaraka, majarida, tasnifu za awali na kutazama na kusikiza makala ya mtandao wa YouTube. Ufafanuzi wa kimaelezo kwa kuzingatia nadharia ulitumiwa kutolea matokeo ya utafiti ambayo yamewasilishwa kwenye vijimada vilivyomo katika sura tano za tasnifu hii. Matokeo ya utafiti huu yanatoa mchango katika taaluma ya fasihi kwa wahakiki na wanafunzi kufahamu nafasi ya vipengee hivi katika hotuba. Aidha, unawafaidi wahakiki na watafiti wa fasihi kwa kuwaelekeza jinsi ya kuhakiki hotuba.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Cookie settings
  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback