Repository logo
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
Repository logo
  • Communities & Collections
  • All of DSpace
  • English
  • Català
  • Čeština
  • Deutsch
  • Español
  • Français
  • Gàidhlig
  • Italiano
  • Latviešu
  • Magyar
  • Nederlands
  • Polski
  • Português
  • Português do Brasil
  • Suomi
  • Svenska
  • Türkçe
  • Tiếng Việt
  • Қазақ
  • বাংলা
  • हिंदी
  • Ελληνικά
  • Yкраї́нська
  • Log In
    New user? Click here to register.Have you forgotten your password?
  1. Home
  2. Browse by Author

Browsing by Author "Masinde, Edwin"

Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Mashairi huru: uchambuzi wa dhamira na mtindo
    (2012-05-08) Masinde, Edwin
    Tasnifu hii inashughulikia baadhi ya mashairi huru ya watunzi atatu wa tanzania. Inajadili dhamira na mtindo katika mashiri huru ya kiswahili, hususa jinsi dhamira zinavyoathiri uteuzi wa ligha katika kazi ya fasihi na hasa ushairi. Tumejaribu kuonyesha kwamba dhamira ya mtunzi na mtindo anaotumia katika kutoa ujumbe wake ni vipengele vinavyotegemeana. Mtunzi atunga kutokana na tajriba aliyopata katika mazingira yake na lugha ndiyo njia aitumiayo kuyaeleza mambo mbalimbali ya jamii yake kea njia ya kubuni. Mazingira ya mwandishi katika ujumla wake huathiri uteuzi wake wa ligha na mitindo anayoitumia . Katika tasnifu hii, tumejaribu kuonyesha uwiano huu na kudhihirisha kwamba ijapokuwa ushairi huru unatofautianal katika muundo wa nje na ushairi wa jadi, sifa za aina hizi mbili za ushairi ni sawa hasa tukiazingatia umbo la ndani. Aidha tumejaribu kunyesha kuwa mtindo wa mwandishi huathiri uibushaji wa ujumbe wake. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao ni muhtasari wa mwongozo uliotusaidia katika utafiti na uchambuzi wa mashairi-huru tuliyochagua. Kati ya mambo ambayo yamejadiliwa katika sehemu hii ni somo la utafiti, madhumuni ya utafiti na msingi wa nadharia. Pia tumeeleza upeo wa tasnifu na kujadili kazi mbalimbali ambazo zimeshughulikia somo hili. Sura ya pili inajadili mazingira walimotungia washairi tuliowachagua. Tunaafiki maoni ya Senkoro (1987: 1) kwamba misingi na mikondo ya historia ya jamii huipa fasihi umbo kimaudhui na kifani pamoja na mwelekeo. Rene Wellek na Austin Warren (1949: 94-95) wanasisitiza kauli hii kwa kusema: - Fasihi ni asasi ya kijamii inayotumia lugha; ni ubunifu wa Kijamii. Vipengele vya fasihi kama taswira na mdundo vinatokana na jamii. Wahakiki hawa wanachosisitiza ni kwamba fasihi haiibuki katika ombwe tupu. Hivyo, mhakiki wa fasihi hana budi kuzingatia mazingira ya kijamii ili kugundua vipengele vinavyoihuisha kazi fulani. Ni katika muktadha huu ambapo tunasisitiza kwamba mazingira ya kihistoria ya Tanzania, yawe ya kijamii, kiuchumi au kisiasa, yameathiri kazi za washairi hawa kidhamira na kimtindo. Ushairi kama kazi ya sanaa utaeleweka na kutathminiwa vyema zaidi katika mazingira ya wakati maalum wa kihistoria. Pia fasihi hupata uhai wake kutokana na hali halisi za jamii. Hivyo basi katika sura hii, tumejadili mazingira ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Watanzania katika vipindi viwili muhimu; wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni. Tumejadili kipindi cha uhuru katika viwango viwili: Kabla na baada ya Azimio la Arusha la mwaka 1967. Lengo letu hapa ni kuonyesha jinsi matukio muhimu katika vipindi hivi yalivyoathiri mifumo ya kijamii ya Watanzania na kuathiri fasihi yao katika vipengele vyote. Katika sura ya tatu, tumechambua mashairi yenye maudhui ya kisiasa. Tumeonyesha jinsi maudhui ya mtunzi yalivyosababisha uteuzi maalum wa lugha katika kuyaibusha. Sura ya nne imejadili uchambuzi wa mashairi yenye maudhui ya uchumi. Katika sehemu hii, tumeonyesha jinsi uteuzi wa mtindo maalum wa mwandishi unavyosaidia kuibusha dhamira na jinsi dhamira pia inavyoathiri uteuzi huu. Katika sura ya tano, tumechambua mashairi yenye maudhui ya maswala mengine ya kijamii kama vile ndoa, mapenzi, dini, utamaduni na falsafa kuhusu maisha. Tumeonyesha namna maudhui hayo yalivyojengwa kifani. Imedhihirika kwamba umbo la ndani la shairi ni muhimu katika kueleza maana yake. Sura ya sita ni hitimisho. Sura hii ni muhtasari wa matokeo ya utafiti wetu ambamo licha ya kueleza ugunduzi wa uchambuzi wetu, tumetoa kauli yetu juu ya ushairi-huru na mashairi-huru, na maeneo ambayo yanastahili kufanyiwa utafiti zaidi hapo baadaye.
  • Loading...
    Thumbnail Image
    Item
    Umuhimu wa Vipengele vya Kiisimu katika Kuendeleza Kazi ya Mashairi Huru
    (East African Journal of Swahili Studies, 2025-04) Wafula, Pouline Nangila; Masinde, Edwin
    Makala hii imelenga kuchunguza umuhimu wa vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili katika diwanı teule za Kithaka wa Mberia na Kezilahabi. Diwani teule zilizochanganuliwa ni: Doa, Mvumo wa Helikopta, Msimu wa Tisa, Kichomi na Karibu Ndani. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani ambayo iliasisiwa na Liberman (1975) na kuendelezwa na Liberman na Prince (1977), Nadharia ya Fonolojia mizani inadai kuwa mkazo katika lugha uko katika mfumo wa mfuatano wiani wa kimsonge ambao hupanga silabi maneno na virai katika sentensi. Vipengele vya kiisimu vilivyochanganuliwa ni: aina za sentensi, kipengele cha nafsi na uakifishaji. Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimakusudi katika kuteua diwani teule. zilizohakikiwa. Data Iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani. Ni Maktabani ndiko tuliweza kusoma mashairi kutoka katika diwani teule, nadharia ya utafiti na vitabu vingine vinavyohusiana na mada ya utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mbinu ya uhakiki matini kwa kuongozwa na pengo la utafiti. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo yaliyoambatanishwa na mifano ya beti mwafaka za mashairi kutoka katika diwani teule. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa vipengele vya isimu vinachangia pakubwa katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili. Utafiti lengwa umechangia katika taaluma ya ushairi kwa kuelewa umuhimu wa vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili. utafiti huu unapendekeza wasomaji wa mashairi, huru wazingatie matumizi ya vipengele vya kiisimu katika kuendeleza kazi ya mashairi huru ya Kiswahili.

DSpace software copyright © 2002-2026 LYRASIS

  • Cookie settings
  • Privacy policy
  • End User Agreement
  • Send Feedback