MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Alice Nyambura Mwihaki"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Lugha ya wanawake wakikuyu inavyoimarishwa ubabedume katika maongezi ya kawaida(2012-03-29) Muchiri, Patrick Maina; Alice Nyambura Mwihaki; Miriam Kenyani OsoreUtafiti huu ulilenga kubainishajinsi wanawake Wakikuyu wanavyouimarisha ubabedume kupitia maongezi yao ya kawaida. Nadharia ya Tahakiki Usemi imekuwa nanga ya uchanganuzi wa matumizi ya lugha kutokana na msisitizo wake wa muktadha katika kueleweka kwa matamshi. Sarufi Amilishi Mfumo imejaliza uchanganuzi kupitia msisitizo wake wa mfumo wa maana za matamshi. Utafiti ulifanywa maktabani na pia nyanjani. Maktabani, data ya upili ilitumiwa ili kufanikisha utafiti wa nyanjani. Nyanjani, maongezi halisi ya wanawake kuhusu wanaume yalizingatiwa hasa sokoni, na kwenye vikundi vya wanawake. Uwasilishaji wa data utakuwa wa kimaelezo kupitia sura tano. Sura ya kwanza imejenga utangulizi ikihusisha vipengele vya kimsingi vya utafiti. Utamadunijamii wa Wakikuyu umeshughulikiwa katika sura ya pili pamoja na vipengele vyake vinavyokuza ubabedume. Taswira ya mwanamume na taswira ya mwanamke zimefafanuliwa na mifano halisi ya kimaongezi kutolewa katika sura ya tatu na ya nne mtawalia. Ufafanuzi wa maana za taswira hizi ulikitwa katika miktadha ya matumizi ya lugha kama inavyoelekeza nadharia inayotumiwa katika utafiti huu. Sura ya tano imehitimisha utafiti kwa kutoa matokeo ya utafiti, mahitimisho ya utafiti pamoja na mapendekezo ya utafiti zaidi. Utafiti huu unatarajiwa kuwanufaisha wanaisimu, wasomi wa masuala ya kijinsia, na wanawake kwa jumla. Pia unatarajiwa kusaidia katika uzinduzi wa jamii kuhusu matumizi ya lugha na athari zake kimawasiliano.Item Uchanganuzi semantiki wa maneno mkopo ya kikamba kutoka kiswahili(2011-11-15) Mumbua, David Jane; Alice Nyambura Mwihaki; Mbaabu, I. G.Utafiti huu ulidhamiria kuchanganua mchakato wa kisemantiki kwa kuegemea maneno mkopo ya Kikamba kutoka Kiswahili. Uchanganuzi huu hasa ulilenga kubainisha kanuni zinazotawala taratibu mbalimbali za utohozi maana. Tafiti awali zimeangazia zaidi utohozi fonolojia na utohozi mofolojia bila kuzingatia kanuni katika mchakato wa utohozi maana. Aidha kazi hii ilinuia kufidia upungufu wa tafiti awali kwa dhamira ya kupanua ufahamu zaidi katika mfumo wa maana, na semantiki ya Kikamba. Utafiti ulifuata nadharia msingi ya Tahakiki Usemi na kushirikisha Sarufi Amilishi Mfumo. Kwa jumla nadharia hizi hutazama lugha kama mfumo wenye maana na unaodhibitiwa na mfumo wa kijamii. Utafiti huu pia ulihusisha njia mbili kuu za utafiti: utafiti wa nyanjani na ule wa maktabani. Tasnifu ya utafiti imewasilishwa kwa njia ya maelezo, mifano na vielezo katika sura nne. Sura ya kwanza maswala ya kimsingi yanajitokeza: usuli wa mada, swala la utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, tahakiki ya maandishi, misingi ya nadharia na uchanganuzi wa data. Sifa za kifonolojia, kimofolojia na kisemantiki zimeangaziwa katika sura ya pili yaani muundo wa maneno ya Kikamba. Matokeo kuhusu taratibu za utohozi semantiki na kanuni husika katika maneno mkopo yaliyochanganuliwa yamefafanuliwa katika sura ya tatu. Jumla ya mahitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo ya utafiti yamejadiliwa katika sura ya nne. Imani na falsafa za kijamii ni miongoni mwa maswala yaliyodhihirika kuelekeza maana za maneno mkopo.