MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Ahutah, Tony Munyasa"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Upekee wa Lugha Katika Mikahawa ya Eastlands(2012) Ahutah, Tony Munyasa; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu ulilenga kutambua na kubainisha sifa zinazoifanya lugha ya mikahawani- Eastlands kuwa na upekee fulani. Hizi ni sifa ambazo zimekita hadi kiwango cha kuifanya lugha hii ielekee kuwa namna ya sajili ya mikahawa hii inayopatikana mashariki mwa jiji la Nairobi. Tumechanganua data kutoka kwa mikahawa sita inayopatikana katika mitaa ya Jericho, Maringo, Bahati; eneo la mashariki mwa Nairobi. Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu. Malengo haya yalikuwa: kubainisha sifa zinazobainisha lugha ya mikahawa ya Eastlands, kutambua maana zinazowasilishwa na lugha inayotumiwa mikahawani na jinsi lugha asili za wakazi zinavyoathiri lugha inayotumiwa mikahawani humo. Katika utafiti wetu tumeongozwa na nadharia ya sarufi amilifu mfumo iliyoasisiwa na Halliday miaka ya 1960. Nadharia hii huchunguza lugha kimuktadha. Kwa mujibu wa nadharia hii ya sarufi amilifu mfumo, lugha ina dhima ya kuelezea tajiriba zetu na kuzipatanisha tajiriba hizo ili kuunda matini inayoleta maana inayokusudiwa. Tumeitumia nadharia hiyo kuchanganua maana katika muktadha wa mazingira ya mikahawani, muundo na mwingiliano wa matini. Ripoti ya utafiti huu imepangwa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi, ya pili imeshughulikia sajili kwa jumla, na ya tatu imeangazia lugha mikahawani Eastlands. Sura ya nne imeshughulikia maana mbalimbali zinazojitokeza katika matini na ya mwisho ni mahitimisho, matokeo ya utafiti na mapendekezo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwa lugha ya mikahawa Eastlands ina sifa bainifu kama vile: utohozi wa maneno, kuchanganya msimbo, kubuni nomina kutoka kwa vitenzi na kuunganisha nomino kuvitaja vyakula. Aidha, utafiti huu umeonyesha kuwa lugha ya mkahawani ina maana tatu tofauti. Maana hizi ni maana dhanishi, maana tagusani na maana matinishi. Katika muundo wa matini kauli za kuamuru, maswali, ufupisho maagizo na vishazi vinatumiwa. VI