MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Adero, Margan, Carlpeters"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uwezo wa Lugha katika Matini ya Siasa Nchini Kenya Kuanzia Mwaka 2002 hadi 2005.(2014-03-13) Adero, Margan, Carlpeters; Ryanga, Sheila; Mbaabu, I. G.Utafiti huu unaangazia uwezo wa iugha katika matini ya siasa nchini Kenya. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kudhihirisha vile lugha hutumiwa na wanasiasa ili waweze kuonyesha itikadi zao na pia kupata mamlaka. IIi kuonyesha uwezo wa lugha katika matini za siasa nadharia ya uchanganuzi usemi hakiki ndio imetumiwa. Katika utafiti huu sura ya kwanza ambayo ni utangulizi wa tasnifu inashughulikia swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, nadharia, madhumuni, upeo wa utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Sura ya pili inaangazia na kueleza dhana muhimu zilizotumiwa katika utafiti. Pia inaelezea mwingiliano uliopo kati ya lugha, siasa, mamlaka na itikadi. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa data ya hotuba za kisiasa na kuzichanganua kimuktadha na kimaana. Inatoa maelezo ya hotuba zilizotolewa katika kipindi cha siasa kinachozungumziwa. Sura ya nne ni uchanganuzi wa data na kueleza uwezo huo wa lugha katika hotuba za kisiasa nchini Kenya. Sura ya tano ni matokeo ya utafiti, mapendekezo ya utafiti mwingine na matatizo yaliyoukumba utafiti.