PHD-Department of Kiswahili & African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing PHD-Department of Kiswahili & African Languages by Author "Momanyi, Clara"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Uainishaji wa ushairi wa Kiswahili:Dhima ya methali(2013-01-22) Maitaria, Joseph Nyehita; Momanyi, Clara; Wafula, Richard M.Utafiti huu umeshughulikia dhima ya methali katika kuainishia ushairi wa Kiswahili. IIi kufanikisha lengo hilo, uchanganuzi umefanywa kwa kuzingatia tungo mahususi za Said Ahmed Mohamed (2001), Kithaka wa Mberia (2001), Alamin Mazrui (1994), Akilimali Snow-White (1974), Euphrase Kezilahabi (1974) na Abdilatif Abdalla (1974). Hao ni miongoni mwa watunzi mashuhuri wa ushairi wa Kiswahili hapa Afrika Mashariki kuanzia mwaka wa 1970 hadi wakati wa sasa. Mihimili iliyoongoza utafiti huu ilitokana na nadharia mbili: Fomula ya Kisimulizi na ile ya Semiotiki. Aidha, utafiti ulifanywa maktabani na nyanjani. Tasnifu hii imegawanyjka katika sura saba. Sura ya kwanza, imeshughulikia mada na madhumuni ya utafiti. Udurusu wa maandishi yaliyohusu mada ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia iliyoongoza utafiti huu pia iliigusiwa. Sura ya pili, imeshughulikia namna methali zilivyotumiwa kama fomula katika uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili. Maelezo hayo yameimarisha utathmini wa uwiano uliopo baina ya fani na maudhui katika mashairi hayo teule. Nayo sura ya tatu, imechanganua baadhi ya mashairi ya Akilimali Snow-White na ya Abdilatif Abdalla ili kufafanulia dhima ya methali katika ushairi uliozingatia arudhi za kimapokeo. Sura ya nne, imechanganua baadhi ya mashairi ya Said Ahmed Mohamed na ya Alamin Mazrui. Uchanganuzi huo umebainisha jinsi ushairi wa kati ulivyotumia methali chache na ulivyoshirikisha kauli zilizoibuliwa kwa makusudi. Kadhalika, sura ya tano imechanganua baadhi ya mashairi ya Kithaka wa Mberia na ya Euphrase Kezilahabi ili kubainisha mwelekeo kuhusu matumizi ya methali chache mno au kutotumiwa kwazo katika uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili. Aidha, sura hiyo imedhihirisha dhima ya methali kupitia kwa maudhui yaliyowasilishwa. Sura ya sita, imebainisha uainishaji wa Ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia matumizi ya methali. Uainishaji huo umependekeza kuwa ushairi wa Kiswahili huweza kugawanywa zaidi kimakundi. Sura ya saba, ni hitimisho la tasnifu. Mambo muhimu ambayo yamezingatiwa ni pamoja na muhtasari, matokeo, matatizo na mapendekezo kuhusu jinsi ushairi wa Kiswahili unavyoweza kufanyiwa utafiti zaidi. Aidha, sura hiyo imejaribu kujibu maswali ya utafiti kulingana na uchanganuzi wa mashairi yaliyozingatiwa..Item Usawiri wa mwanamke Muislamu katika jamii ya waswahili kama inavyobainika katika ushairi wa Kiswahili(2012-04-10) Momanyi, ClaraUtafiti huu umeshughulikia usawiri wa mwanamke muislamu katika jamii ya Waswahili kama inavybainika katika kazi za washairi walioteuliwa. Lengo kuu la utafiti huu ni kuhakiki tungo za washairi walioteuliwa ili kuona jinsi mwanamke anavyosawiriwa katika ushairi huo. Ili kufanikisha lengo hili, uchanuzi wa tungo za Muyaka Bin Haji, Mwanakupona Binti Mshamu na Shaaban Robert unemfanywa. Nadharia iliyoongoza utafiti huu inatambuliwa kama Uchanguzi-nafsia katika mtazamo wa kike. Nadharia hii huzingatia mahusiano ya kiuana na jinsi mahusiano haya yanavyowasilishwa katika kazi za fasihi. Aidha, nadharia hii huchunguza jinsi utaratibu wa kijamii unavyochangia kumweka mwanamke katika kitengo maalumu. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na sababu za kuchagua mada hii. Udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia iliyoongoza utafiti huu pia yamegusiwa. Sura ya pili inahusu historia na utamaduni wa waswahili Waislamu, itikadi na mitazamo yao. Maelezo haya ni muhimu katika kuimarisha msingi bora wa kuelewa yale yanayosawiriwa na Washairi walioteuliwa katika utafiti huu. Sura ya nne inachanganua Utendi wa Mwanakupona. Uchanganuzi huo umebainisha jinsi mwanamke anavyojitokeza kulingana na itikadi zilivyojitokeza katika Utendi huo. Ainisho la majukumu ya mwanamke kama inavyobainika katika utendi huu linatuwezesha kuona picha halisi ya mwanamke katika wakati wa Mwanakupona. Sura ya tano inahakiki ushairi wa Shaaban Robert ili kubainisha taswira ya mwanamke na nafasi aliyotengewa na jamii. Sura hii inajadili msimamo wa mwandishi kuhusu swala la mwanamke kulingana na mabadiliko yaliyoikumba jamii ya wakati wake. Sura ya sita ni hitimisho la tasnifu hii. Mambo makuu yaliyozingatiwa ni pamoja na muhtasari, matokeo, matatizo na mapendekezo ya mtafiti. Sura hii inayajibu maswali ya utafiti kulingana na matokeo ya uchanganuzi wa mashairi yaliyoteuliwa.