Uainishaji wa ushairi wa Kiswahili:Dhima ya methali

Loading...
Thumbnail Image
Date
2013-01-22
Authors
Maitaria, Joseph Nyehita
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia dhima ya methali katika kuainishia ushairi wa Kiswahili. IIi kufanikisha lengo hilo, uchanganuzi umefanywa kwa kuzingatia tungo mahususi za Said Ahmed Mohamed (2001), Kithaka wa Mberia (2001), Alamin Mazrui (1994), Akilimali Snow-White (1974), Euphrase Kezilahabi (1974) na Abdilatif Abdalla (1974). Hao ni miongoni mwa watunzi mashuhuri wa ushairi wa Kiswahili hapa Afrika Mashariki kuanzia mwaka wa 1970 hadi wakati wa sasa. Mihimili iliyoongoza utafiti huu ilitokana na nadharia mbili: Fomula ya Kisimulizi na ile ya Semiotiki. Aidha, utafiti ulifanywa maktabani na nyanjani. Tasnifu hii imegawanyjka katika sura saba. Sura ya kwanza, imeshughulikia mada na madhumuni ya utafiti. Udurusu wa maandishi yaliyohusu mada ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia iliyoongoza utafiti huu pia iliigusiwa. Sura ya pili, imeshughulikia namna methali zilivyotumiwa kama fomula katika uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili. Maelezo hayo yameimarisha utathmini wa uwiano uliopo baina ya fani na maudhui katika mashairi hayo teule. Nayo sura ya tatu, imechanganua baadhi ya mashairi ya Akilimali Snow-White na ya Abdilatif Abdalla ili kufafanulia dhima ya methali katika ushairi uliozingatia arudhi za kimapokeo. Sura ya nne, imechanganua baadhi ya mashairi ya Said Ahmed Mohamed na ya Alamin Mazrui. Uchanganuzi huo umebainisha jinsi ushairi wa kati ulivyotumia methali chache na ulivyoshirikisha kauli zilizoibuliwa kwa makusudi. Kadhalika, sura ya tano imechanganua baadhi ya mashairi ya Kithaka wa Mberia na ya Euphrase Kezilahabi ili kubainisha mwelekeo kuhusu matumizi ya methali chache mno au kutotumiwa kwazo katika uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili. Aidha, sura hiyo imedhihirisha dhima ya methali kupitia kwa maudhui yaliyowasilishwa. Sura ya sita, imebainisha uainishaji wa Ushairi wa Kiswahili kwa kuzingatia matumizi ya methali. Uainishaji huo umependekeza kuwa ushairi wa Kiswahili huweza kugawanywa zaidi kimakundi. Sura ya saba, ni hitimisho la tasnifu. Mambo muhimu ambayo yamezingatiwa ni pamoja na muhtasari, matokeo, matatizo na mapendekezo kuhusu jinsi ushairi wa Kiswahili unavyoweza kufanyiwa utafiti zaidi. Aidha, sura hiyo imejaribu kujibu maswali ya utafiti kulingana na uchanganuzi wa mashairi yaliyozingatiwa..
Description
Department of Kiswahili & African Languages, 590p. 2012, PL 8010.4.M3
Keywords
Citation