Umahuluti wa Miundo katika Tamthilia za Ebrahim Hussein
dc.contributor.author | Okwena, Sophie | |
dc.date.accessioned | 2020-10-06T06:47:17Z | |
dc.date.available | 2020-10-06T06:47:17Z | |
dc.date.issued | 2019 | |
dc.description | Tasnifu Hii Imewasilishwa katika Idara ya Kiswahili, Shule ya Fani na Sayansi za Kijamii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa Ajili ya Kutimiza Mahitaji ya Shahada ya Uzamifu, 2019 | en_US |
dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia umahuluti wa miundo katika tamthilia za Ebrahim Hussein. Matumizi ya miundo anuwai katika tamthilia za Hussein ndilo suala lililochochea utafiti huu. Tamthilia zilizochanganuliwa ni tano ambazo ni Kinjeketile (1969), Mashetani (1971), Jogoo Kijijini (1976), Ngao ya Jadi (1976) na Arusi (1980). Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo: Kuchunguza iwapo maisha na elimu ya Ebrahim Hussein yaliweza kuathiri utunzi wake. Kuchunguza sifa za kimahuluti zinazopatikana katika tamthilia ya Kinjeketile. Kubainisha miundo ya kimahuluti inayojitokeza katika tamthilia za Mashetani na Arusi. Kutathmini vipengele vya kimahuluti katika tamthilia za Jogoo Kijijini na Ngao ya jadi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia tatu changamano ambazo ni nadharia ya ki-Hegel ya mwaka wa 1882 ambayo iliasisiwa na Georg Friedrich Hegel inayojadili masuala ya kipembuzi. Nadharia ya ki-Brecht iliyoasisiwa na Bertolt Brecht mwaka wa 1924 ambayo inaangazia masuala ya ukengeushi. Nadharia ya ki-Propp ya Fomyula ya Kisimulizi ambayo iliasisiwa na Vladimir Propp mwaka 1939 inashughulikia masimulizi ya Kiafrika. Nadharia hizi zilifaa utafiti huu hasa ikizingatiwa kwamba Hussein ametumia miundo anuwai katika tamthilia zake. Mbinu kusudio na mbinu ya utabakishaji zilitumika katika kuteua sampuli lengwa ambayo ni tamthilia tano teule. Nyanjani, waliohojiwa waliteuliwa kimakusudi na kila kundi liliwakilishwa na watu watatu yaani, wahakiki watatu na waandishi wa tamthilia watatu. Vifaa vya aina mbili vilitumika: maswali ya mwongozo wa mahojiano na mjadala. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kwamba, kuna chembechembe za umahuluti katika tamthilia za Ebrahim Hussein. Uchanganuzi ulionyesha kwamba, mwingiliano wa Ebrahim Hussein na tamaduni mbalimbali ulimfanya kushirikisha miundo tofauti tofauti katika kazi zake. Waaidha, kuishi kwake na kuingiliana na tamaduni tofauti, kumemfanya kuchukua vipengele vya tamaduni hizo na kuvifanya kuwa vipengele muhimu katika maisha yake na katika kazi zake za kiubunifu. Hivyo, Hussein anashirikisha miundo ya kidrama ambayo ilichimbuka kutokana na usomaji wa maandishi tofauti tofauti. Utafiti huu umechangia katika kufahamu upekee wa kazi za Ebrahim Hussein kwamba, hakuna fasihi halisi yaani, fasihi ya Kiswahili ni mahuluti katika vipengele vyake vyote. Pia, utafiti ulichangia katika kufafanua baadhi ya sifa za fasihi ya Kiafrika, Kimagharibi na ya kisasa, jambo ambalo huonyesha jinsi watu huingiliana na mwingiliano huu huwaathiri kiasi cha kuzalisha fasihi mahuluti. Kadhalika, utafiti ulikuwa wa manufaa zaidi katika uwanja wa fasihi kwa sababu uliwanufaisha wahadhiri pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kuhakiki kazi zao. | en_US |
dc.description.sponsorship | Chuo Kikuu cha Kenyatta | en_US |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/20532 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.publisher | Kenyatta University | en_US |
dc.title | Umahuluti wa Miundo katika Tamthilia za Ebrahim Hussein | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Umahuluti Wa Miundo Katika Tamthilia…………………………..pdf
- Size:
- 1.37 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full Text Thesis
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: