Uhusiano wa mikakati ya ufundishaji wa fasihi ya watoto ya kiswahili na umilisi wa kusoma katika shule za msingi, kasarani, kaunti ya Nairobi, Kenya
Loading...
Date
2016-10
Authors
Chacha, Selina Rhobi
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
IKISIRI
Fasihi ya watoto ina manufaa katika ukuzaji wa umilisi wa lugha shuleni na hata
katika mazingira ambayo si ya shule. Licha ya manufaa hayo, baadhi ya wanafunzi
hawasomi vitabu vya hadithi. Kutopenda kusoma kunaweza kuwa kumesababishwa
na mikakati inayotumiwa na walimu katika ufundishaji wa vitabu hivyo vya fasihi.
Lengo la utafiti huu ni kuchanganua mikakati inayotumiwa katika ufundishaji wa
fasihi na umilisi wa kusoma miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi za ya
Kasarani. Utafiti huu ulichanganua vifaa vya kufundishia na kutathmini kazi ya
wanafunzi. Aidha, utafiti uliongozwa na nadharia ya semiotiki ambayo hujengwa
kwa miundo ishara. Mwanzilishi wa nadharia semiotiki alikuwa Charles Piece.
Muundo wa utafiti huu ulikuwa wa usoroveya elezi. Mbinu bahatishi ilitumiwa
kuteua shule za msingi za umma wilayani Kasarani. Mbinu kusudi ilitumiwa
kuteua walimu wa Kiswahili kumi na wawili wanaofundisha darasa la saba. Mbinu
bahatishi ilitumiwa kuteuwa wanafunzi sitini katika kila darasa. Insha sitini za
wanafunzi katika shule ziliteuliwa na kuchanganuliwa ili kutathmini umilisi wa
kusoma miongoni mwa wanafunzi. Vifaa vilivyotumiwa katika utafiti ni hojaji na
mahojiano kwa walimu, kutazama somo darasani na kutathmini insha za
wanafunzi. Data ilichanganuliwa kwa kutumia tarakilishi, ili kupata uwiano na
wastani. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa kutumia maelezo, majedwali na
michoro. Kutokana na utafitii, asili mia moja ya walimu waliripoti kuwa kusoma
kwa kimya na wa kipekee ni mikakati mikuu wanayoitumia kufunza fasihi. Utafiti
pia ulibaini kuwa, asili mia moja ya walimu walitumia vitabu vya hadithi na ubao
katika ufundishaji. Vifaa vya teknolojia ya kisasa havikutumiwa. Matokeo ya
utafiti huu yalionyesha kuwa wanafunzi hawakufanya vizuri katika insha zao
kwasababu walimu hawakutumia mikakati tofauti tofauti na vifaa vya teknolojia ya
kisasa. Walimu wanatakikana kutumia mikakati tofauti tofauti na vifaa vya
teknolojia ya kisasa katika ufundishaji ili kuimarisha matokeo ya lugha ya
Kiswahili. Utafiti huu ulikuwa wa manufaa kwa walimu, wanafunzi, wakuzaji
mitaala na watafiti wa fasihi ya watoto.
ABSTRACT
Children literature is an important aspect in children’s language performance in
school and life after school. Despite its critical role, pupils are not reading enough
literature books for them to master language. The purpose of this study was to
analyse the teaching strategies used to teach children literature and reading
competence among class seven pupils at Kasarani Sub-County, Nairobi County.
The study aimed at achieving the following objectives: to analyse the teaching
strategies used by teachers to teach children literature; to analyse resources used in
teaching children literature; and to evaluate children’s reading comptence in
literature. This research was guided by Semeotic Theory. The design of the study
was descriptive survey. Simple random sampling was used to sample twelve
schools in Kasarani and purposive sampling was used to select twelve Kiswahili
teacher’s handling children literature in class seven. Questionnaires, interview
guides, observation and document analysis were used to collect data. The collected
data was edited, organized, entered into a computer and analyzed with the aid of
Social Package for Social Sciences (SPSS). The analysed data was presented using
descriptive statististics such as tables, graphs and charts. The findings of this study
indicated that silent and individual reading were the major strategies used in
teaching liteature in most primary schools, thus, teachers did not use variety of
teaching strategies. All teachers (100%) agreed that story books and writing
boardswere the major resources used in delivering children literature. The study
concludes that new instructional techniques such as redio lessons, televisions,
recorded videos and audios were not utilized at all. Majority of pupils, as well, did
not perform well in all sections of composition.This is because the teachers did not
use different strategies and new instructional techniques in their teaching to
improve pupils performance. The study recommends that; teachers should use
different strategies in teaching children’s literature, children should be encouraged
to read more story books, and library lessons should be more than one
Description
Tasnifu hii imewasilishwa kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika idara ya mawasiliano na teknolojia ya elimu, shule ya elimu, Chuo Kikuu cha Kenyatta. October, 2016 Call No. PL 8703.5 .K4C48
Keywords
Swahili literature