Taswira za kiuana katika nyimbo za tohara za wanaume miongoni mwa Waigembe
Loading...
Date
2011-11-07
Authors
Kobia, John Mwithalii
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ni uchunguzi wa taswira za kiuana katika nyimbo za tohara za wanaume miongoni mwa Waigembe, nchini Kenya. Utafiti umehakiki majukumu, itikadi na mahusiano ya kiuana katika jamii ya Waigembe kupitia uchunguzi wa mojawapo ya tanzu za fasihi simulizi yao: nyimbo za tohara. Taswira za wanaume na wanawake katika nyimbo za tohara za wanaume zimehakikiwa ili kuibuka na mwonoulimwengu unaokubalika katika jamii ya Waigembe kuhusu mwanamume na mwanamke katika jamii hii. Misingi ya kinadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya mtazamo wa kimwingiliano. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya uana kwa misingi ya maoni ya wataalamu kama vile Cameroon (1985), Coates (1985), Ostergeerd (1992), Meena (1992); nadharia ya uamali kama inavyopendekzwa na Levinson (1983) na Horn (1991); nadharia ya viwango vya manna kwa muj ibu wa Turner (1967) na nadharia ya utendaji kwa mtazamo wa Fine (1984), Schechner (1988) na Foley (1995). Nadharia ya uana imefaidi katika uhakiki wa taswira za mwanamume na mwanamke zinazoj itokeza katika nyimbo za tohara. Nadharia ya uamali ni muhimu katika uchanganuzi wa matumizi ya lugha katika muktadha wa utendaji wa nyiso. Nadharia ya viwango vya manna imetumika katika uhakiki wa maana mbalimbali, ilhali nadharia ya utendaji imesaidia katika uchanganuzi wa suala la utendaji, hadhira na uumbuji wa kimawasiliano katika nyimbo za tohara katika jamii ya Waigembe.
Data asilia na iliyorekodiwa imetumika katika utafiti huu. Ili kupata misingi ya nadharia za uana, uamali, viwango vya manna na utendaji pamoja na usuli wa Waigembe na fasihi simulizi yao hasa nyimbo; maktaba, makavazi na tovuti mbalimbali zilitembelewa. Kwa kutumia mbinu za uchunguzi shirikishi nyanjani, hojaji, mahojiano ya kibinafsi na ya vikundi, data asilia ilikusanywa kutoka kata ndogo tisa (9) katika tarafa ya Igembe Mashariki, wilayani Igembe, mkoa wa Mashariki. Kwa kutumia mbinu ya usampuli matilaba (makusudi), wahojiwa 36 ambao ni magwiji wa fasihi simulizi ya Waigembe, (wanaume wawili na wanawake wawili kutoka kila kata ndogo), walishiriki katika utafiti huu. Data asilia iliyokusanywa (nyimbo za tohara za wanaume) ilirekodiwa kwenye kanda za kaseti na kanda ya video; kuandikwa kwa Kiigembe na kutafsiriwa kwa Kiswahili. Maneno yalifasiriwa kimuktadha ili kupata maana katika taswira za kiuana zinazodhihirika katika nyimbo hizo. Taswira za mwanamume na mwanamke zilihakikiwa kwa mujibu wa misingi ya nadharia za uana, uamali na viwango vya maana. Uchanganuzi wa taswira ulimwongoza mtafiti katika kutoa kauli na hoja katika utafiti huu. Imebainika kuwa nyimbo za tohara katika jamii ya Waigembe hutumia taswira kisanii ili kudhihirisha itikadi ya kiuana ya Waigembe, kukemea nwvu ya kijamii, kufichua na kuwakejeli waliopotoka kimaadili katika jamii. Utafiti unatoa wito kwa wanajamii kuzinduka katika matumizi ya fasihi simulizi ya Kiafrika, kama chombo cha maendeleo kinachotambua wanaume na wanawake, siyo wapinzani, bali kama washiriki katika maendeleo.