Mofologia ya maneno mkopo ya Gikuyu kutoka Kiswahili: Mtazamo wa fonolojia Leksia.

dc.contributor.advisorMwihaki, A.N.
dc.contributor.advisorGathenji, H.W.
dc.contributor.authorWaithaka, Njeri Margaret
dc.date.accessioned2011-08-11T09:33:07Z
dc.date.available2011-08-11T09:33:07Z
dc.date.issued2011-08-11
dc.descriptionDepartment of Educational Management, Policy and Curriculum Studies,155p.The PL 8379 .W32 2010
dc.description.abstractSuala la manenomkopo hupatikana katika taaluma ya Isimu Linganishi Historia. Utafiti uliolengwa ulichanganua utohozi mofologia wa manenomkopo ya Gikuyu kutoka kiswahili kwa madhumuni ya kubainisha kanuni na taratibu zilizohusika. Manenomkopo hujitokeza yakiwa na sura mbalimbali za mofologia ya lugha inayokopa. Madhumuni ya utohozi ni kuyafanya manenomkopo yalingane na kuafiki mfumo wa lugha pokezi. Tafiti za awali kuhusu utohozi hazijashughulikia utohozi mofolojia kwa kina kwa kutumia misingi ya nadharia. Uchanganuzi wa maendeleo ulitegemea mtazamo wa fonologia Leksia katika nadharia ya fonologia inayozingatia falsafa ya sarufi zalishi. Kulingana na mtazamo huu, uambishaji wa maneno umengaliwa kwa jumla na mageuzi ya maumbo ya maneno yanadhibitiwa na sheria za kifonologia. Data msingi ilikusanywa kutoka miktadha mbalimbali ya matumizi ya lugha kama vile nyumbani, sikoni, redioni na kanisani. Mbinu ya uchunguzi ilikuwa kushiriki, mazungumzo na kusikiliza. Katika kuwasilisha, maelezo yaliambatanishwa na michoro, vielezo na jedwali. Taratibu za kimofologia zilizohusika katika utohozi ziliangaziwa. Aidha, uchunguzi ulikuwa na nafasi kubwa y akuchangia usomi wa kiswahili na Isimu za lugha za Kiafrika kwa jumla. Zaidi ya hayo, utafiti huu ulibainisha tofauti kati ya Gikuyu na kiswahili ingawa zote ni lugha za Kibantu. Kazi hii ingerejelewa na wasomi wa baadaye hasa kuhusu utohozi wa manenomkopo kwa jumla.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/707
dc.language.isootheren_US
dc.subjectKikuyu language --Foreign words and phrases
dc.subjectSwahili language --Kenya
dc.subjectBantu languages --Kenya
dc.subjectKikuyu language --Morphology
dc.subjectKikuyu language --Phonology
dc.titleMofologia ya maneno mkopo ya Gikuyu kutoka Kiswahili: Mtazamo wa fonolojia Leksia.en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mofolojia ya Manenomkopo......pdf
Size:
62.6 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: