Mielekeo ya walimu na wanafunzi kuhusu mbinu na mazingira ya ufundishaji na athari kwa matokeo ya Kiswahili, Kisumu na Kakamega, Kenya
Loading...
Date
2024-11
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Idara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Elimu Chuo Kikuu Kiswahili ni lugha rasmi na ya taifa nchini Kenya ambapo ni somo la lazima linalofundishwa na kutahiniwa katika shule za msingi na za upili. Kimataifa, ni lugha inayotambuliwa kama chombo cha mawasiliano. Umilisi wa lugha hii hubainishwa kupitia ujuzi wa mtu katika stadi zake kuu; kusikiliza kuongea, kusoma na kuandika. Umilisi na utendaji katika lugha hata hivyo huweza kuathiriwa pakubwa na mielekeo ya mtu kuhusu lugha husika, wazungumzaji wake au hata majukumu yake.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wanafunzi wengi hawawezi kujieleza kwa usahihi na kwa ufasaha hata baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili. Hali hii ilimchochea mtafiti wa kazi hii kuchunguza mielekeo ya walimu na wanafunzi wa shule za upili kuhusu mbinu na mazingira ya ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza mchango wa mielekeo ya wanafunzi na walimu katika ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika Kaunti za Kisumu na Kakamega. Utafiti huu ulidhamiria: Kubainisha mitazamo kuhusu lugha ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na walimu katika Kaunti za Kisumu na Kakamega, kuchunguza visababishi vya mitazamo hii, kuchunguza namna mitazamo hii ilivyoathiri shughuli ya ufunzaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili na iwapo ilikuwa na mchango wowote katika matokeo ya mitihani yake. Misingi ya nadharia iliyotumiwa ni ya nadharia za tabia na utambuzi. Utafiti huu ulitumia mbinu changamano; ulifuata mtindo wa kidahilishi na utaratibu wenye maelezo, kijarabati pamoja na utaratibu wa ulinganuzi. Wasailiwa walikuwa ni wakuu wa idara ya Kiswahili, walimu walioteuliwa kimaksudi na wanafunzi wa kidato cha tatu walioteuliwa kimaksudi na kinasibu katika shule za umma zilizoteuliwa kimakundi na kinasibu. Vifaa vya utafiti vilivyotumika ni hojaji, mahojiano, mitazamo ya darasani na mtihani wa Insha. Data ilichanganuliwa kutumia Toleo la takwimu 13 kwa muundo wa kimaelezo, kijarabati au kiidadi na kuwasilishwa kwa kutumia asilimia, grafu, viwango vya urudiaji na pai chati. Matokeo ya utafiti huu yalibainishwa kimaudhui kulingana na madhumuni yake. Kutokana na matokeo ya ANOVA, vigeu vya kaunti, eneo la shule, umri na mwelekeo yalikuwa na umuhimu tofauti wa kiwango cha p<0.05 isipokuwa jinsia kwa kiwango cha p>0.05 kuonyesha kuwa zilizokuwa na umuhimu (kaunti, eneo la shule, umri na mwelekeo) ziliathiri matokeo ya wanafunzi japo tofauti iliyokuwepo ilikuwa ni finyu sana; huenda ilitokea kibahati. Kwa mujibu wa matokeo ya Urejeshaji wa vifaa (Logistic regression), matokeo ya wanafunzi wa Kisumu yalionyesha kuwa walikuwa na uwezekano wa 0.57 wa kuwa wabunifu zaidi kuliko Kakamega bali shule za mijini zilikuwa 1.79 wabunifu zaidi kuliko wa mashambani. Wanafunzi waliokuwa na mielekeo chanya walikuwa na uwezekano wa 1.45 wa kuwa wabunifu zaidi kuwaliko wenye mielekeo hasi. Makadirio ya walimu na wakuu wa idara yaliwiana kuhusu visababishi vya mielekeo kama kusahihisha kwa 62% bali yalitofautiana katika vigeu vingine kama ufaafu wa vifaa, vipindi walivyovifunza katika wiki, mada za somo kulingana na mahitaji yao, ya jamii na mielekeo ya wanafunzi; ambavyo walimu waliyakadiria sana kuliko wakuu hawa. Kulingana na wanafunzi mielekeo yao ilisababishwa sana na jinsia (90.1%) na eneo la shule (88.2%). Katika kaunti zote zaidi ya 50% ya wanafunzi walibainisha kuwa kelele ilikuwa changamoto kwao, chini ya 40% walikosa vifaa vya kutosha vya kujifunzia na muda wa kudurusu. Isitoshe, chini ya 20% walikubali kukosa watu wa kuiga pamoja na waelekezi somoni. Kulingana na walimu, kaunti zote zilibainisha kwa zaidi ya 90% kuwa uzembe wa wanafunzi ulikuwa changamoto kuu.Tofauti ya kimielekeo kati ya Kisumu na Kakamega si bayana sana kama ilivyo kati ya shule za mashambani na ya mijini huku wa mijini wakiwa na mielekeo chanya zaidi kuhusu lugha; mijini kwa 56.7% na mashambani 46.4% na mbinu za ufunzaji na ujifunzaji; mijini kwa 55.9% na mashambani 46.4%. Maoni ya walimu kulingana na athari ya mielekeo katika ufunzaji na ujifunzaji yalikadiriwa kuwa sawa Kisumu na mashambani kuwa viwango vya wanafunzi ndicho kisababishi kikuu kwa 100%, kikifuatwa na mielekeo ya wanafunzi (91.7%) na muda uliopo (91.7%). Hata hivyo, shule za Kakamega na mijini zilikadiria kwa njia sawa kuhusiana na mambo haya. Kakamega ilikadiriwa zaidi kuhusiana na mielekeo ya walimu huku Kisumu ikiongoza katika mambo mengine. Kulingana na wakuu wa idara, Kakamega inaonyesha kinyume cha hali ilivyokuwa Kisumu; Kisumu ikidokeza mielekeo ya wanafunzi kwa 75% Kakamega ikiwa na 45.4% huku mielekeo ya walimu Kisumu ikiwa chini; 41.7% na Kakamega 75%. Kuna mapendekezo kadhaa yaliyotolewa kuhusu namna ya kuimarisha ufunzaji na ujifunzaji wa Kiswahili na kuboresha matokeo yake katika mitihani hasa ya kitaifa nchini. cha Kenyatta
Description
Tasnifu hii imewasilishwa kwa minajili ya kutosheleza mahitaji ya shahada ya uzamifu katika elimu ya lugha, kitivo cha elimu, chuo kikuu cha kenyatta
Novemba, 2024
Wasimamizi:
Profesa John N. Kimemia
Daktari Sophia M. Ndethiu