Maana za majina ya watu katika jamii ya wakamba

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-08-09
Authors
Musyimi, Muendi Dorcas
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umedhamiria kuchunguza maana, ishara-maana na misingi ya kitamaduni ya majina ya watu katika jamii ya Wakamba. Pamoja na kuwa majina huwa na maana wazi, pia kung maana fiche ambayo huashiria matukio fulani katika jamii hii. Mtafti ametumikiza nadharia ya Semiotiki. Kulikuwa na haja ya utafiti huu ill kufidia pengo lililopo katika semantiki hasa uchanganuzi wa maana za majina ya watu katika jamii hii. Wilaya ya Machakos, Makueni, Mwingi na Kitui ndizo zilizokuwa maeneo ya utafiti. (Tazama kiambatisho 1). Data iliyotumika ilikusanywa maktabani na nyanjani, kwa kutumia mbinu ya hojaji wazi. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia maswali ya utafiti na misingi y a nadharia. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maandishi. Tasnifu hii imepangwa katika sura nne. Sura ya kwanza imesheheni maswala ya kimsingi kama vile: usuli wa mada, swala la utafiti, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada, misingi ya nadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pill imezungumzia jamii ya Wakamba na mfumo wao wa majina. Sura ya tatu imeshughulikia uchanganuzi wa data na matokeo yake. Sura ya nne imetoa muhtasari wa utafiti, changamoto na mapendekezo ya utafiti zaidi. Uchunguzi huu utawafaa wanaanthropolojia, wanasosiolojia, wanaisimu na pia jamii ya Wakamba na makundi mengine ya watu ulimwenguni katika kuurejelea na kuuendeleza utamaduni wao.
Description
Abstract
Keywords
Citation