MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Chanzo cha Taharuki"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Utata kama Chanzo cha Taharuki Katika Vichwa vya Habari Katika Gazeti la Taifa Leo(Kenyatta University, 2023) Njeru, Joyce Wanjiru; leonard chacha mwitaUtafiti huu ulidhamiria kutathmini utata kama chanzo cha taharuki katika vichwa vya habari katika gazeti la Taifa Leo. Pia, utafiti huu ulilenga kuweka wazi athari ya utata uliopo katika vichwa vya habari kwa wasomaji wa gazeti la Taifa Leo. Gazeti ni njia mwafaka na muhimu ya kuwasilisha ujumbe kama vile masuala nyeti, sera za serikali, masuala ibuka na ujumbe mwingine wowote. Wasomaji ndio wapokezi wa habari hizo. Hivyo, ni muhimu kuchunguza athari ya utata huo kwa wasomaji kwani ndio walengwa. Nia ya wahariri wa gazeti ni kupitisha ujumbe. Vichwa vya habari ni sehemu muhimu ya kuwapa wasomaji msukumo wa kusoma habari zilizopo katika gazeti na hivyo, vichwa vinapaswa kuibua taharuki ili kuvutia wasomaji wasome ujumbe huo. Hivyo basi, utafiti huu ulilenga kuchunguza iwapo vichwa vya habari vyenye utata vinaibua taharuki katika gazeti la Taifa Leo. Taharuki ilichukuliwa kuwa, hamu ya kutaka kujua yanayofafanuliwa katika habari baada ya kusoma kichwa fulani cha habari, yaani msukumo ambao huchochea wasomaji kutaka kujua kinachozungumziwa katika habari inayofuata. Pia, utafiti huu uliweza kuweka bayana maoni ya wasomaji wa gazeti la Taifa Leo kuhusiana na utata katika vichwa vya habari. Nadharia iliyotumiwa katika utafiti huu ni nadharia ya maana kama matumizi iliyoasisiwa na Wittgenstein mwaka wa 1930 ambayo ilituelekeza kuchunguza maana ya maneno katika muktadha wa mutumizi yake. Utafiti huu ulifanywa maktabani na nyanjani. Maktabani, mtafiti alisoma vitabu na majarida yaliyo jadili kuhusu utata na kuchambua vichwa vya habari vyenye utata katika gazeti la Taifa Leo ili kubainisha aina mbalimbali za utata. Utata uliobainika katika data iliyokusanywa ni utata wa kileksia, utata wa kimantiki, utata wa kutafakari, utata wa kipragmantiki na utata wa kisarufi. Nyanjani, wasomaji, wahariri na waandishi wa gazeti la Taifa Leo walihojiwa ili kutathmini athari ya utata uliopo katika vichwa vya habari na iwapo utata huo huzua taharuki kwa wasomaji. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa asilimia kubwa ya wasomaji huwa na athari chanya kuhusu utata katika vichwa vya habari na vichwa hivyo huzua taharuki kwa wengi wa wasomaji wa gazeti la Taifa Leo. Hata hivyo, ilibainika kuwa wakati mwingine utata uchanganya na kupotosha ujumbe lengwa na hivyo kutozua taharuki kwa wasomaji. Hivyo, wahariri wanapaswa kuwa makini wanapoteua vichwa vya habari ili vizue taharuki. Utafiti huu utawasaidia waandishi na wahariri wa gazeti kutambua athari na maoni ya wasomaji kuhusiana na vichwa vya habari vyenye utata na mchango wa utata katika kuzua taharuki. Hili litawasaidia kuwasilisha ujumbe ipasavyo wakitilia maanani wasomaji wa gazeti. Pia, utafiti huu utapanua fikra za wasomaji kuhusu utata katika vichwa vya habari kwa kuwa uliweza kuchambua utata kwa kina.