MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "British Broadcasting Corporation"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Tathmini ya Hadithi Fupi Zilizowasilishwa Katika British Broadcasting Corporation: Mtazamo wa Edgar Allan Poe na Leech (1969)(Kenyatta University, 2021) Macharia, Francis Maina; Richard Wafula; Pamela M. Y. NgugiUtafiti huu umetathmini hadithi fupi zilizowasilishwa katika BBC kwa kuzingatia mtazamo wa Edgar Allan Poe. Katika kufanya hivyo, mtafiti amejihusisha na uhakiki wa mikusanyiko: Mapenzi ni Kikohozi (1970), Vituko Duniani (1970), Pavumapo Palilie (1971) na Kinywa Jumba la Maneno (1977) za kipindi kati ya 1970 hadi 1977 maarufu kama “Hekaya za Kuburudisha” zilizochapishwa na shirika la Longman Kenya wakishirikiana na BBC. Mikusanyiko hii inajumuisha hadithi ambazo zilitokea kuwa bora na hivyo zikasomwa hewani na shirika la utangazaji la BBC na hatimaye zikachapishwa kwanzia 1970 hadi 1977. Mtafiti amezingatia mtazamo wa Edgar Allan Poe (1842; 1846) na kipengele cha uhakiki cha mtindo katika kutalii hadithi hizi na kukadiria usanii wa watunzi wa hadithi fupi teule. Kwa kufanya hivyo, ametathmini hadithi fupi zilizowasilishwa katika BBC. Nadharia ya uhakiki ya mtindo pamoja na misingi ya hadithi fupi iliyowekwa na Poe (1842; 1846) imetumika katika kufanikisha utafiti huu. Leech na Short (1981) wanafafanua mtindo kama namna mwandishi anavyotumia lugha kuzingatia muktadha maalumu na kwa lengo mahsusi. Mtindo ni ule upekee wa kujieleza katika maandishi au mazungumzo. Poe (1842; 1846) anaweka misingi ya hadithi fupi kwa kuorodhesha vigezo muhimu ambavyo vinafaa kuzingatiwa ili kufanya hadithi fupi kuvutia na kuwa bora. Nadharia ya mtindo na misingi iliyowekwa na Poe imesaidia katika kutathmini hadithi fupi zilizoko katika mikusanyiko hii ya awali zaidi. Mbinu ya utafiti iliyotumika ni ya kimaelezo ikirutubishwa kwa kiasi fulani na mbinu ya kitakwimu. Mbinu ya kimaelezo imetumika pale ambapo mtafiti amedondoa sentensi au matukio ya kimaelezo na kuchanganua hadithi teule. Aidha, mbinu ya kitakwimu imetumika wakati wa kuteua hadithi mbalimbali kutoka mikusanyiko ya hadithi fupi tuliyoorodhesha. Sampuli imeteuliwa kimaksudi. Utafiti umekuwa wa maktabani. Inatarajiwa utafiti huu utakuwa na mchango hasa kwa upande wa muundo, maudhui na usawiri wa wahusika katika mtindo kwa kuonyesha namna hadithi fupi inastahili kusukwa ili kuwafaa waandishi chipukizi katika kusanii kazi zenye ubora wa muundo, mtindo na maudhui.