MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Bahati Bukuku"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Uchanganuzi wa Usimulizi Kama Mtindo Katika Nyimbo za Bahati Bukuku(Kenyatta University, 2021) Aboge, Asige Nelson; Pamela M. Y. Ngugi; Peter GithinjiUtafiti huu ulichunguza vipengele vya usimulizi katika nyimbo teule za Bahati Bukuku. Nyimbo aghalabu huwa na mbinu za kimtindo ambazo huwasilisha jinsi maudhui yalivyojitokeza katika nyimbo hizo. Uhakiki huu ulijikita katika vipengele vitatu; mitindo ya simulizi kwa kuzingatia ploti na wakati, suala la maudhui pamoja na uchanganuzi wa sauti ya usimuliaji na mahusiano ya wakati wa usimulizi. Maswali ya utafiti yalikuwa; ni kwa njia gani mbinu ya masimulizi katika uimbaji imejitokeza katika nyimbo za Bahati Bukuku kuzingatia ploti na wakati? Je, mbinu ya usimulizi imesaidia vipi katika kutambua maudhui katika nyimbo za Bahati Bukuku? Je, vipengele vya sauti ya usimuliaji na mahusiano ya wakati wa usimulizi imedhihirika vipi katika nyimbo teule za Bahati Bukuku? Utafiti huu una malengo matatu ambayo ni; kueleza jinsi usimulizi katika nyimbo imejitokeza kwa kuzingatia vipengele vya ploti na wakati, kudhihirisha usimulizi kama njia ya kuwasilisha maudhui na pia kufafanua jinsi vipengele vya sauti ya usimuliaji na mahusiano ya wakati wa usimulizi vimejitokeza katika nyimbo teule za Bahati Bukuku. Nadharia iliyotumika ni ya Naratolojia inayojumuisha usimulizi katika tanzu za fasihi. Nadharia hii hujumuisha usimulizi katika tanzu kama vile nyimbo, mashairi, maghani na kadhalika. Suala kuu katika nadharia hii ni simulizi na usimulizi na pia uhakiki wa ploti kama kipengele muhimu cha usimulizi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa katika ukusanyaji wa data pale ambapo uteuzi wa nyimbo zilizotumiwa katika utafiti ulitokana na kanda za video tepetevu za nyimbo za injili za Bahati Bukuku. Data yenyewe ilinakiliwa kwa kurejelea malengo ya utafiti na msingi wa nadharia husika. Utafiti wa maktabani ulitumika katika kukusanya data kupitia usomaji wa vitabu, majarida, makamusi, tasnifu za awali pamoja na makala ya mtandaoni yaliyosaidia katika kuafikia malengo ya utafiti huu. Hii ni baada ya kununua albamu zinazosheheni nyimbo za Bahati Bukuku, pamoja na kutoa nyimbo zingine mtandaoni, kuzisikiliza na kuzihakiki kulingana na malengo ya utafiti. Utafiti huu utawafaa watafiti wa baadaye katika kazi zao za kuhakiki mada zinazohusiana na utafiti huu. Vilevile utafiti huu utachangia katika kuonyesha jinsi mbinu ya kimtindo ya usimulizi inavyoweza kufanikisha uwasilishaji wa maudhui kwa wasikilizaji wa nyimbo hizi kwa kuzingatia nyimbo zilizoimbwa kwa kutumia mtindo huu. Hali hii itafanikishwa kupitia hadithi ambazo zimeweza kujitokeza katika nyimbo za Bahati Bukuku ambazo zimeweza kuwasilishwa kwa kaida za utambaji wa hadithi. Utafiti huu pia utawafaa watafiti wa baadaye ambao tahakiki zao zitaandikwa kwa kutumia nadharia ya naratolojia.