MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Subject "Athari"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Athari za Ekegusii Katika Matumizi ya Kiimbo cha Kiswahili Miongoni mwa Wanafunzi wa Shule za Upili Kaunti ya Kisii, Kenya(Kenyatta University, 2023-11) Nyougo, Christine; Peter GithinjiUtafiti huu ulichunguza matumizi ya kiimbo cha Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza. Shule tatu zilihusishwa katika utafiti huu: Shule ya upili ya Senior Chief Musa Nyandusi, Nyamondo na Nyabisia. Malengo ya utafiti huu yalikuwa: Kutathmini utamkaji na ufasili wa kiimbo cha Kiswahili miongoni mwa wanafunzi wanaozungumza Ekegusii kama lugha ya kwanza, kuchunguza jinsi viarudhi vya lugha ya Ekegusii vinavyoathiri kiimbo cha Kiswahili. Kutathmini jinsi usuli wa lugha na tajriba ya wanafunzi inavyochangia matumizi bora ya kiimbo katika uzungumzaji wa Kiswahili. Ili kuafiki madhumuni haya, maswali yafuatayo yalitumiwa: Je, wazungumzaji wa Ekegusii hufasili vipi kiimbo cha Kiswahili sanifu? Viarudhi vingine vya Ekegusii huathiri kiimbo cha Kiswahili vipi? Usuli na tajriba ya wanafunzi huchangia vipi katika matumizi bora ya kiimbo cha Kiswahili? Nadharia ya ujifunzaji wa kiimbo cha lugha ya pili iliyoasisiwa na Mennen (2015) ilitumiwa katika kuchunguza matumizi ya kiimbo. Utafiti huu ulifanywa maktabani na nyanjani. Maktabani ulihusu kusoma matini, vitabu, tasnifu, majarida na makala mtandaoni kuhusu kiimbo. Nyanjani ulijumuisha matumizi ya hojaji funge na wazi katika kupata tathmini ya wanafunzi ya sampuli ya data waliyopewa na mtafiti. Vilevile, mbinu ya mahojiano ambayo yalirekodiwa ilitumika kwa walimu wanaofunza Kiswahili. Pia, uchunzaji wa kushiriki ulitumiwa. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo, majedwali, michoro na chati. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa lugha ya Ekegusii huathiri matumizi ya kiimbo sahihi cha Kiswahili. Wazungumzaji wa Ekegusii walionyesha athari katika usomaji na ufasili wa kiimbo cha Kiswahili. Ilibainika kuwa viarudhi vingine vya Ekegusii huathiri matumizi ya kiimbo cha Kiswahili. Utafiti ulithibitisha kuwa jinsia huchangia katika matumizi sahihi ya kiimbo ambapo ilidhihirika kuwa jinsia ya kike hutumia kiimbo sahihi katika mazingira rasmi ikilinganishwa na jinsia ya kiume. Tajriba pia huchangia kiimbo sahihi pale ambapo wanafunzi ambao wamekuwa shuleni kwa muda mrefu huzungumza kwa kiimbo bora. Vifaa vya kisasa pia huchangia kuboresha matumizi ya kiimbo sahihi cha Kiswahili. Tunapendekeza walimu wakuze matumizi ya vifaa vya kisasa katika ufundishaji wa kiimbo cha Kiswahili, kuwepo sheria shuleni kuhusu matumizi ya Kiswahili katika mazingira rasmi na ufundishaji wa kiimbo utiliwe maanani kuanzia viwango vya chini vya elimu.Item Athari za Matukio ya Kihistoria Katika Riwaya za Nyongo Mkalia Ini na Mafamba(Kenyatta University, 2022-04) Ndung’u, Beatrice Wanjiku; Richard Wafula; Jessee MurithiThis research study investigated the effect of historical events on the selected two novels Nyongo Mkalia Ini (Chimerah, 1995) and Mafamba (Olali, 2008). The effects of historical events that include political, administrative, economic and social issues in general and how they affect the presentation of themes, characters and style and language is an issue that has not been addressed as a specific research research topic in the novel. The aim of this research has been to investigate whether historical events affect how novelists portrays themes in their literary works, investigate how historical events affect characterization and investigate how historical events affect the linguistic styles in swahili novel. The research has employed new historicism theory which was founded by Greenblatt (1980). New historicism theory puts into consideration contextual importance in composing and analyzing literary work. The theory also stipulates that, as the society develops; cultural changes occur that consequently affects composition, depiction and analysis of literary works. The topic on effect of historical events to the development of Swahili novel is important for various reasons. This research has been done in the library through reading the selected novels, journals and prior literary works relevant to the research. Research findings have be presented through analysis and explanations. The research has been presented in five chapters. The research has shown the effects of historical events on Nyongo Mkalia Ini and Mafamba. The research has shown that historical events have affected writers in depicting their themes, characters and linguistic styles in Nyongo Mkalia Ini and Mafamba respectively.