PHD-Department of Kiswahili & African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing PHD-Department of Kiswahili & African Languages by Subject "Swahili literature//Muslim women"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri wa mwanamke Muislamu katika jamii ya waswahili kama inavyobainika katika ushairi wa Kiswahili(2012-04-10) Momanyi, ClaraUtafiti huu umeshughulikia usawiri wa mwanamke muislamu katika jamii ya Waswahili kama inavybainika katika kazi za washairi walioteuliwa. Lengo kuu la utafiti huu ni kuhakiki tungo za washairi walioteuliwa ili kuona jinsi mwanamke anavyosawiriwa katika ushairi huo. Ili kufanikisha lengo hili, uchanuzi wa tungo za Muyaka Bin Haji, Mwanakupona Binti Mshamu na Shaaban Robert unemfanywa. Nadharia iliyoongoza utafiti huu inatambuliwa kama Uchanguzi-nafsia katika mtazamo wa kike. Nadharia hii huzingatia mahusiano ya kiuana na jinsi mahusiano haya yanavyowasilishwa katika kazi za fasihi. Aidha, nadharia hii huchunguza jinsi utaratibu wa kijamii unavyochangia kumweka mwanamke katika kitengo maalumu. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na sababu za kuchagua mada hii. Udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia iliyoongoza utafiti huu pia yamegusiwa. Sura ya pili inahusu historia na utamaduni wa waswahili Waislamu, itikadi na mitazamo yao. Maelezo haya ni muhimu katika kuimarisha msingi bora wa kuelewa yale yanayosawiriwa na Washairi walioteuliwa katika utafiti huu. Sura ya nne inachanganua Utendi wa Mwanakupona. Uchanganuzi huo umebainisha jinsi mwanamke anavyojitokeza kulingana na itikadi zilivyojitokeza katika Utendi huo. Ainisho la majukumu ya mwanamke kama inavyobainika katika utendi huu linatuwezesha kuona picha halisi ya mwanamke katika wakati wa Mwanakupona. Sura ya tano inahakiki ushairi wa Shaaban Robert ili kubainisha taswira ya mwanamke na nafasi aliyotengewa na jamii. Sura hii inajadili msimamo wa mwandishi kuhusu swala la mwanamke kulingana na mabadiliko yaliyoikumba jamii ya wakati wake. Sura ya sita ni hitimisho la tasnifu hii. Mambo makuu yaliyozingatiwa ni pamoja na muhtasari, matokeo, matatizo na mapendekezo ya mtafiti. Sura hii inayajibu maswali ya utafiti kulingana na matokeo ya uchanganuzi wa mashairi yaliyoteuliwa.