Browsing by Author "Mwita, Leonard Chacha"
Now showing 1 - 2 of 2
Results Per Page
Sort Options
Item Jinsi Leksimu za Mitishamba Zinavyoakisi Uhifadhi wa Mazingira ya Waswahili Nchini Kenya(East African Journal of Swahili Studies, 2023) Karoli, Nelly Bonareri; Mwita, Leonard ChachaLugha na utamaduni wa watu ni vitu visivyoweza kutenganishwa. Mifumo ya lugha huathiri namna binadamu anavyofikiri kuhusu ulimwengu wake na husababisha matendo ambayo ni kiini cha changamoto za kiikolojia wanazokabiliana nazo. Katika makala hii, tulichambua namna leksimu za mitishamba zinachukuliwa kama ishara za uhifadhi wa mazingira katika mifumo ya ikolojia katika jamii ya Waswahili. Data ilikusanywa kwa mbinu ya mahojiano kutoka kwa Waswahili wa Mvita. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya semiotiki ikolojia iliyotusaidia kuelewa kuwa kile kilichotambuliwa kama athari kwa ikolojia mara nyingi huwa na sababu za kisemiotiki na tofauti katika kufasiri ishara au misamiati. Tulibainisha kuwa kuna leksimu za mitishamba kama ‘mpambamwitu’ ambayo Waswahili walitumia kuonyesha ile hali ya kurembesha misitu yao kwa kuleta taswira ya kiasili na mwonekano mzuri wa kipekee, ‘linda ziwa’ iliakisi uhifadhi wa vyanzo vya maji. Mahali ambapo ulimea, maji yalikuwa safi na tayari kutumika katika shughuli za pale nyumbani. Mti huu ulifananishwa na jokofu kwani hata nyakati za joto ulipoenda mtoni ungepata maji hayo ni baridi na safi. Waswahili ambao walikuwa ni watumiaji wa leksimu hizi walionyesha kuwa ilipofikia suala la uhifadhi wa mazingira, wanajamii walijitahidi kutunza mazingira yao. Jinsi tunavyochagua misamiati yetu katika mawasiliano kuhusu mazingira kunaweza kubadilisha jinsi wanajamii wanavyoyaona mazingira hayo. Ikolojia inategemea mawazo yaliyopo, kanuni, na sheria za jamii. Makala hii imapendekeza kuwa kwa kubadilisha jinsi tulivyoyatazama mazingira yetu ya asili tunaweza kutambua thamani yake halisi. Kwa kuiweka thamani hiyo katika sera zetu mipango na mifumo ya uchumi, tunaweza kuelekeza uwekezaji katika shughuli ambazo zinarejesha uasili wa mazingira yetu na tukapata faida. Kwa kutambua kuwa mazingira yetu ni mshirika wetu mkubwa basi tutayafanya kuwa endelevu.Item Polisemi ambazo Zimeundwa Kutokana na Sitiari na Metonimu katika Kiswahili(EANSO, 2024-02) Masika, Mark Elphas; Mwita, Leonard ChachaMakala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili. Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi . Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu. Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu.