Browsing by Author "Muthoni, Reuben Wahome"
Item Usimulizi kama Kipengele cha Muundo Unavyojitokeza kwenye Diwani ya Akiba ya Wema Iliyohaririwa na Timothy Arege(EANSO, 2026-01) Muthoni, Reuben Wahome; Muriithi, Jesse JosephUtafiti huu ulichunguza usimulizi kama kipengele cha muundo kwenye Diwani ya Akiba ya Wema ambayo imehaririwa na Timothy Arege. Malengo ya utafiti huu yalikuwa pamoja na kubainisha sauti za usimuliaji na viwango vya usimulizi vinavyotumika katika Diwani ya Akiba ya Wema iliyohaririwa na Timothy Arege, Kuonyesha nafasi ya wakati katika usimulizi wa hadithi kwenye diwani hii, kudhihirisha uwasilishaji wa usemi na fikra za wahusika katika uendelezaji wa hadithi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Naratolojia ambayo ilianzishwa na mwasisi Plato na baadaye kuendelezwa na wengine kama: Propp (1968), Claude (1970), Barthes (1975), Todorov (1977), Genette (1980), Bal (1999) na Fludernik (2009). Nadharia hii hutumika kuchunguza jinsi matukio hufuatana kwenye hadithi fulani. Utafiti huu ulichunguza usimulizi kwa nadharia hii kuegemea mwelekeo wa Genette (1980). Vigezo vya nadharia hii vilivyozingatiwa ni sifa za muundo wa usimulizi na vipengele vyake kuzingatia uamilifu au uhusiano uliopo kiwakati na kiusemi. Utafiti ulikuwa umejikita maktabani ambapo, vitabu, majarida, tasnifu na makala ambayo yanahusu usimulizi yalisomwa. Mbinu ya usampulishaji makusudi ilitumika katika kukusanya data iliyotokana na waandishi tofauti kuhusu usimulizi. Asilimia 40 ya sampuli kuhusu usimulizi ilitumika kwenye hadithi ambazo ni 13 hivyo hadithi 5. Mafungu yanayoonyesha fikra za wahusika na miundo mbali mbali ya hadithi mahsusi yalidondolewa kwenye sampuli ya hadithi tano zilizochaguliwa.