Browsing by Author "Mohammed, Hawa Kabura"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Mwingilianomatini katika Riwaya Teule za Mwenda Mbatiah(Kenyatta University, 2024-09) Mohammed, Hawa Kabura; King'ei, Kitula Osore, MiriamUtafiti huu ulichunguza mwingilianomatini katika riwaya za Mwenda Mbatiah. Utafiti ulijikita katika riwaya tatu: Upotevu (1999), Msururu wa Usaliti (2011) na Watoto wa Mwelusi (2018). Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha mazingira ya mtunzi yalivyochangia maingiliano katika riwaya teule, kudhihirisha kuingiliana kwa maudhui kulivyojitokeza katika riwaya teule na kutathmini usawiri wa wahusika ulivyoingiliana katika riwaya za Mwenda Mbatiah. Nadharia ya mwingilianomatini ndio ilitumika. Nadharia hii ilianza kujitokeza katika karne ya ishirini, mwanaisimu Ferdinand de Saussure alipoibuka na nadharia ya ishara. Alieleza ishara za kiisimu hupata maana kwa kurejelea ishara za awali. Misingi ya nadharia hii ilipatikana katika nadharia ya usemezano ya Bakhtin (1981) na kuendelezwa na Julia Kristeva aliyekuwa wa kwanza kutumia neno mwingilianomatini mwaka wa 1960. Nadharia ya mwingilianomatini husisitiza kuwa matini haiwezi kujisimamia na hutegemea matini nyingine ya hapo awali. Mihimili mikuu ilikuwa, matini hutegemea aina mbalimbali za tamaduni zilizowekwa na kazi asilia pale maisha ya kawaida huunganishwa kisha kubadilishwa, matini huwa ni kijalizo cha matini tangulizi kwani kauli huandikwa upya kwa kudokeza, mwangwi, kuiga na kuibadili kulingana na muktadha mwingine wa kijamii na upokezi na uwelewekaji hutegemea matini tangulizi kwani maana ya matini hupatikana kwa kutegemea matini nyingine. Nadharia ilisaidia kuonyesha jinsi mazingira ya kihistoria, kijamii na kiuchumi hufanya kazi za mwandishi mmoja kuingiliana na kupiga mwangwi katika kazi zake. Riwaya ziliteuliwa kimakusudi kwa vile zilisaidia kupata data iliyotakikana ya kujaza pengo. Data ya kimsingi ilikusanywa maktabani kwa kusoma riwaya teule na kunakili vipengele muhimu. Tasnifu, majarida, vitabu pia zilisomwa na kusakura mitandao kusoma kazi zilizotafitia mwingilianomatini. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kutilia maanani malengo ya utafiti, maswali na nadharia ya mwingilianomatini. Utafiti ulisaidia kuonyesha maingiliano yaliyosababisha mwangwi wa masuala muhimu yaliyotokana na mazingira ya kihistoria, kijamii na kiuchumi. Mchango wa utafiti huu ni kuonyesha umuhimu mkubwa wa mwingilianomatinini ni kumwezesha mhakiki na mtafiti kuwa na mikakati mahsusi wa kulinganisha na kulinganua.