MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Catherine Mwihaki Ndungo"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Swala la mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili: waandishi katika njia-panda(2012-05-17) Mule, Katwina; Chacha Nyaigotti-Chacha; Catherine Mwihaki NdungoTasnifu hii ni uhakiki wa swala la mwanamke kama linavyojitokeza katika tamthilia za Kiswahili zilizoandikwa na waandishi wa kike. Tunachunguza taswira zinazojitokeza katika kila mojawapo ya kazi tulizozishughulikia. Kutokana na taswira hizi, tunauchambua msimamo wa mwandishi kuhusu swala la ukombozi wa wanawake. Uchunguzi huu umeibuka kutokana na imani kwamba wanawake ni kundi linalodhulumiwa katika jamii ya sasa kwa msingi ya uana wao. Tunaamini kwamba lazima swala la ukombozi wao lianze nao. Uchunguzi wetu basi unajaribu kunchunguza iwapo waandishi hawa ni watetezi halisi wa maslahi ya wanawake. Sura ya kwanza ni utangulizi. Hapa, tunazingatia somo la utafiti, madhumuni yake na upeo wa utafiti huu. Pia tumezungumzia kwa ufupi yale yalioandikwa kuhusu mada hii na kuelezea kwa muhtasari nadharia tunayoitumia kuzitathmini kazi tulizochagua. Hatimaye tunatoa sababu zilizotufanya kulichagua somo hili na kuonyesha njia tulizotumia kuufanya utafiti huu. Sura ya pili inawachambua waandishi wawili wa kipekee wa Kenya. Hawa ni Sheila Ali Ryanga na Ari Katini Mwachofi. Tumeonyesha kuwa waandishi hawa wanatofautiana kumaudhui, uendelezaji wa wahusika na kimtazamo. Hata hivyo, kwa njia moja au nyingine, wanaonekana kutokuwa na msimamo thabiti kuhusu swala la mwanamke. Sura ya tatu inazichunguza tamthilia mbili za Penina Muhando alizoziandika kati ya 1972 na 1974 na tamthilia moja ya Angelina Chogo aliyoiandika 1976. Hawa ni waandishi wa Tanzania. Tumeonyesha athari za siasa ya ujamaa kwa uchotaji na unendelezaji wa maudhui, wahusika na masuluhisho wanayoyapendekeza kwa matatizo yanayoikumba jamii yao; swala la mwanamke likiwemo. Sura ya nne ni Uchambuzi wa tamthilia mbili za Penina Muhando alizoziandika katika miaka ya themanini. Tumeonyesha jinsi mwandishi huyu anavyobadilika na kupevuka kimtazamo katika kazi hizi zikilinganishwa na zile nyingine za mwanzo. Sura ya tano ndiyo hitimisho ya kazi hii. Hapa, tunatoa muhtasari wa kazi yetu kwa jumla na kujadili kwa ufupi mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hizi. Pia tumetoa mapendekezo yetu kuhusu utafiti zaidi ambao ungefanywa kuwahusu waandishi hawa.