MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Augustine, Muindi"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawini wa wahusika makahaba katika riwaya za Said Ahmed Mohammed(2012-05-17) Augustine, MuindiUtafiti wetu unahusu suala la ukahaba katika riwaya nne za Said Ahmed Mohammed. Tunahakiki usawiri wa wahusika makahaba kwa madhumuni ya kubainisha sababu za kuwepo kwa ukahaba katika jamii. Aidha, tunatalii namna ambavyo mwandishi anawabadilisha wahusika wake kutoka kwa maisha ya ukahaba na kama mabadililo hayo yanatoa suluhisho halisi kwa jamii ya makahaba. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tunapojadili tasnifu kwa jumla, mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti wetu, upeo wa utafiti wetu. Vile vile, tunajadili baadhi ya kazi nyingine zilizowahi kuandikwa na ambazo kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Aidha, tutasema machache kuhusu nadharia tunayotumia katika utafiti wetu. Kisha tutatazama sababu za kuchagua mada hii na njia tutakazofuata katika kutafiti juu ya mada yetu. Katika sura ya pili na ambayo ndiyo nguzo ya utafiti, tunaelezea dhana na nadharia za ukahaba. Dhana na nadharia hizi zinatusaidia katika kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotambulisha kahaba katika jamii. Tunafikia upeo wa utafiti wetu katika sura ya tatu na nne. Katika sura ya tatu, tunanuia kubainisha sababu mbalimbali ambazo zimewavuta baadhi ya wahusika katika maisha ya ukaha ba. Sura ya nne, tunajadili namna ambavyo mwandishi anawaondoa wahusika wake kutoka kwa maisha hayo. Sura ya tano ni ya hitimisho. Tunatoa muhtasari wa kazi tuliyoifanya. Kisha, tunatathmini kama tumefikia malengo ya utafiti wetu. Mwisho tunatoa marejeleo ya utafiti wetu.