MST-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this community
Browse
Browsing MST-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Anaye, Josphat Vonyoli"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Hadithi kama chombo cha maudhui katika fasihi uchanganuzi wa riwaya za Mkangi, G. K. Mafuta (1984) na Walenisi (1995)(2011-12-19) Anaye, Josphat VonyoliUtafiti huu unachanganua hadithi kama chombo cha kutolea maudhui katika riwaya za George Katama Mkangi za Mafuta (1984) na Walenisi (1995). Kwa kutumia nadharia ya uhalisia wa uyakinifu wa kijamaa iliyoasisiwa mwaka wa 1934, miaka michache baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka wa 1917, tumechunguza jinsi Katama Mkangi ametumia urithi wa fasihi simulizi wa jamii yake kutusawiria uhalisi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Utafiti huu umechanganua hadithi tofauti katika riwaya ya Mafuta na Walenisi na kubainisha maudhui ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyojikita katika hadithi hizo. Utafiti huu umeonyesha pia jinsi hadithi za kijadi zimetumiwa kama nyenzo ya kutolea maudhui ya kisasa. Kazi hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi unaojadili suala la utafiti, sababu za kuchagua mada hii, mbinu za utafiti, mapito ya kazi muhimu na misingi ya nadharia. Tungependa kusisitiza kuwa uzito wa utafiti huu umewekwa juu ya hadithi kama chombo cha kutolea maudhui. Hadithi hizi za jadi zimefungamanishwa na uhalisia wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii. Sura ya pili imejadili tanzu za hadithi na umuhimu wake katika riwaya hizi mbili. Sura ya tatu na nne zimechanganua hadithi zinazopatikana katika riwaya za Mafuta na Walenisi na mtindo wa kutolea hadithi katika riwaya hizi mbili. Sura ya Mwisho ni hitimisho ambamo tumebainisha uhusiano na athari baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi na kutoa mapendekezo ya haja ya utafiti zaidi juu ya mitindo anayotumia Mkangi katika riwaya zake.