Riwaya za Kiswahili na Suala la Jinsia: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi’, in Kiswahili na Maendeleo ya Jamii

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Authors
Osore, Miriam
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA)
Abstract
Makala haya yanaangalia suala la jinsia katika riwaya za Said Ahmed Mohamed: Utengano (1980) na Asali Chungu(1977) na za Euphrase Kezilahabi: Rosa Mistika (1971), Kichwa-Maji(1974) na Gamba fa Nyoka (1978). Msimamo wa makala haya ni kwamba, ili kuhakiki suala la jinsia katika riwaya teule kikamilifu, lazima liangaliwe katika misingi ya utamaduni wa Kiafrika. Makala haya yanachukulia kazi ya fasihi kuwa zao la kijamii na lazima ihakikiwe katika misingi namiktadha ya jamii inayohusika. Kwa hivyo, katika kutalii jinsi suala la jinsia lilivyoshughulikiwa na waandis~i hawa, tunatambua umuhimu wa matukio ya kijamii. Msimamo wa makala haya ni kwambamwandishi wa fasihi hueleza hisia na itikadi zake za kibinafsi na falsafa za jamii yake katika fasihi anayoitunga. Katika misingi hiyo, nadharia iliyotumika ni ya uchanganuzi usemi (Critical Discourse Analysis- CDA). Nadharia hii ina waasisi wengi wakiwemo Fowler (1975), (1991), Fairclough (1992), (1995), Van Dijk (1977); (1981) na Wodak (1989). Wote wanasisitiza kwamba matumizi yoyote ya lugha ni kitendoau usemi wa kijamii. Wodak na Meyer (2001) wanaeleza kwamba CDA ni nadharia ya kisasa ambayo haitoi masuluhisho maalum ya masuala yanayomkumba binadamu. Inachukulia kuwa uhakiki wowote na matokeo yake yachukuliwe tu kamajinsi mojawapo ya kuelewa suala fulani. Inalenga kutoa mitazamo mbalimbali ya masuala yanayohusu jamii. Nadharia hii inapendekeza kuwa matumizi ·yote ya lugha ni tukio la kijamii. Katika uhakiki, mhakiki huchanganua miundo yamakala kwa kurejelea sifa zake za kiisimu pamoja na vipengele vya kijamii na vya kitamaduni. Inashikilia kwamba maana kamili ya makala hudhihirika kupitia ushirikiano baina ya vipengele hivi. Inasisitiza kwamba uhusiano baina ya wanajamii huathiri na kudhihirika kupitia kwajinsi wanajamii hawa wanavyozungumza baina yao na kujieleza. Kiujumla makala haya yanashikilia kwamba matumizi yoyote ya lugha yanaelekezwa katika misingi na mipaka ya mfumo wa kijamii na kitamaduni. Ili kupata ujumbe wa Mohamed na Kezilahabi kuhusu suala la jinsia kupitia matumizi yao ya lugha, tunazingatia·mfumo mzima wa kijamii na kitamaduni. Kwa hiyo katika uhakiki wetu, tunajaribu kuonesha uhusiano baina ya usawiri wa suala la j insia katika riwaya teule .na muktadha wa kitamaduni na mifumo ya kiitikadi.
Description
Book Chapter
Keywords
Citation
Miriam Kenyani Osore (2015): ‘Riwaya za Kiswahili na Suala la Jinsia: Mfano wa Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi’, in Kiswahili na Maendeleo ya Jamii edited by Mwenda Mukuthuria et.al. at Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA), Dar es Salaam, TUKI, pp. 32 – 42.