Kutathmini Mafunzo Tafsiri katika Matini za Kidini: Mfano wa Njia Salama
Loading...
Date
2023
Authors
Nyabunga, Vince Arasa
Osore, Miriam
Mwita, Leonard Chacha
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
EANSO
Abstract
Tafsiri imekuwa njia ya kuhamisha maarifa na ujumbe kutoka lugha moja hadi
nyingine kwa muda mrefu lakini imetambuliwa kama taaluma ya kiusomi siyo
miaka mingi iliyopita (Munday, 2001). Tafsiri zilizopo zimefanywa kwa
kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa visawe vya lugha chanzi na lugha
pokezi bila kuhusisha dhana ya uelewaji na ufasiri wa hadhira lengwa. Utafiti
huu ulivuka mtazamo huo na kuchunguza uelewaji na ufasiri wa mafunzo
tafsiri katika Njia Salama. Matini za kidini hutumiwa katika maeneo ya
maabadi ili kuadilisha, kukuza mahusiano na kutangamanisha jamii. Vilevile,
huwasilisha mafunzo muhimu ya kihistoria ya kidini ambayo yanafaa
kueleweka na kufasirika kwa njia ya wazi. Hata hivyo, uchanganuzi wa awali
wa matini tafsiri, unaonyesha kuwepo kwa matatizo ya uelewaji na ufasiri wa
ujumbe wa hali ya maisha na uinjilisti. Kwa hivyo, lengo la utafiti huu ni
kuthamini mafunzo hayo na kubainisha namna matatizo hayo
yanavyojitokeza. Hali kadhalika, utafiti huu unakusudia kuthibitisha iwapo
matatizo ya uelewaji na ufasiri wa ujumbe katika matini teule yanasababishwa
na tofauti za kiisimu, kimtindo, kimuundo na kitamaduni baina ya lugha asilia
na lugha pokezi. Katika kutekeleza jukumu hili, washiriki 140 walishirikishwa
kutoa data ya utafiti. Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa njia ya
kimaelezo na kitakwimu. Kwa hivyo, viongozi 42 na waumini 98 kutoka
kanisa saba teule walishiriki. Washiriki waliojua kusoma na kuandika lugha
ya Kiswahili walisailiwa na kuhojiwa. Nadharia ya skopos inayoweka mkazo
kwenye matini tafsiri iliongoza utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalilenga
kuchangia uelewaji na ufasiri wa ujumbe katika matini tafsiri za kidini
Description
Article
Keywords
Hali ya Maisha, Uinjilisti, Skopos
Citation
Nyabunga, V. A., Osore, M & Mwita, L. C. (2023). Kutathmini Mafunzo Tafsiri katika Matini za Kidini: Mfano wa Njia Salama. East African Journal of Swahili Studies, 6(1), 1-15. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1036.